KARIBU SANA TOSA MAWE BLOG KWA HABARI MBALIMBALI TOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA PIA TUTUMIE HABARI MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +447896103988 +447438590583 | E-mail: mwamfilingef@gmail.com NYOTE MNAKARIBISHWA SANA ASANTENI . | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US CLICK HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Wednesday 28 August 2013

TANZANIA INAHITAJI MAZOEZI MAKUBWA YA KIJESHI,KUNA SABABU YA UGANDA NA RWANDA KUJITOA KUTUMIA BANDARI YA DAR ES SALAAM.

 Rais Museveni Uganda na Kagame Rwanda wanaSIRI yao.
Ninapenda kuzungumzia suala la usalama kwa upande wa nchi za maziwa makuu kama waswahili wanavyosema.Niliwahi kushiriki mkutano wa amani London katika jumba la bunge la Uingereza na kukutana na Profesa kutoka Kongo ambaye alizungumzia suala la Rwanda kushiriki katika mapigano ya Kongo.
Suala lile lilileta hisia kali kiasi kwamba wenzetu weupe walimwita Profesa na kukaa naye kwa maelezo zaidi na kumtaja Kagame anavyotumia wakuu kuongoza waasi wa serikali ya Kongo.
MUHIMU KWA TANZANIA kuajiandaa kwa nguvu zote ili adui aone uwezo na sio kututania tania.Tujifunge mikanda tusione ni mchezo mchezo,hawa jamaa wawili ni marafiki au ndugu wa damu kwa hiyo tusifanye mchezo.
Tukumbuke pia ya IDD AMINI Nyoka  ni kumkata kichwa tu kabla ajaruka na kukuuma
 Katika mkutano huu ulitukutanisha watu kutoka mataifa mbalimbali na ulikuwa na maelezo ya watu wa Kongo wakiomba msaada kwa ajili ya kuwawekea vikwazo Museveni na Kagame.
Profesa katika picha hapo alikuwa akitafuta vielelezo na picha za viongozi wanaoendesha jeshi la waasi wa Kongo kutoka Rwanda.


SYRIA WAJIANDAA KWA KUJIBU MASHAMBULIZI KAMA WATASHAMBULIWA,WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA SYRIA WALID ASEMA KUNA NJIA MBILI ZA KUFANYA KAMA WATASHAMBULIWA 1-KUJIBU MASHAMBULIZI 2-KUJISALIMISHA.MAREKANI YAWEKA MAKAMBORA TAYARI KWA MIJI 50 KUSHAMBULIWA NA NDEGE KUANZA ALHAMISI MASHAMBULIZI.HATARI NYINGINE DUNIANI

Waziri wa mambo ya nje wa Syria , Walid Maullem, amesema anapinga vikali madai kuwa wanajeshi wa serikali ya Syria walitumia silaha za kemikali.
Maullem, aliyasema hayo mjini Damascus, baada ya Marekani kudai kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa silaha za kemikali zilitumika nchini humo.
Bwana Maullem, amesema wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, wameshindwa kufika katika eneo la pili linalodaiwa kushambuliwa kwa silaha hizo, baada ya kuzuiliwa na wapiganaji wa waasi.
Marekani na washirika wake wanajadili uwezekano wa kuanzisha mashambulio dhidi ya Syria kufuatia madai ya shambulio hilo la kemikali lililotokea wiki iliyopita.
Waziri huyo amewaambia waandishi wa habari, kuwa ikiwa nchi yake itashambuliwa kijeshi, kwa misingi ya kuwepo kwa silaha za kemikali, itakuwa kwa visingizio vya uongo na jambo ambalo halina msingo wowote.
Amekariri kuwa serikali ya Syria imetimiza ahadi zote ilizotoa kwa Umoja wa Mataifa kuhusiana na kuruhusu wachunguzi wake kufika nchini humo na pia kuwapa ulinzi
Awali serikali za Urussi na Uchina, kwa mara nyingine tena zimetoa onyo dhidi ya kutumia nguvu za kijeshi kutatua mzozo wa kisiasa unaokumba taifa la Syria.
Onyo hilo limetolewa huku Marekani na washirika wake wakijadili uwezekano wa kuanzisha mashambulio dhidi ya Syria, kujibu shambulio lililotokea wiki iliyopita

MAGAZETI YETU LEO

Monday 26 August 2013

MAUA NI PAMBO LA KUFURAHISHA MOYO WAKO


TANZANIA NCHI YETU INAPOCHEZEA BANDARI,SASA UGANDA NA RWANDA KUACHA KUTUMIA DAR PORT,WAZIRI WETU WA UCHUKUZI ANASEMA NI MWENDA WAZIMA ATAKAYEACHA KUTUMIA BANDARI YA DAR KWANI NI KARIBU UKITUMIA KENYA NI MBALI KWELI ATA KAMA KUNA MATATIZO WATUMIE TU KWELI TUPO PABAYA TUSUBIRI MADHARA YAKE YA AJIRA NA MAPATO,TUSUBIRI TENA CONGO,ZAMBIA NA MALAWI NAO WALIISHA SEMA WATATUMIA MSUMBIJI AU AFRIKA YA KUSINI

Dar es Salaam. Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania (Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.
Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini Serikali haikuchukua hatua.

NAVY READ TO LAUNCH FIRST STRIKE ON SYRIA--VITA VITA VITA DUNIA HII HAKUNA AMANI

Britain is planning to join forces with America and launch military action against Syria within days in response to the gas attack believed to have been carried out by President Bashar al-Assad’s forces against his own people.


MAGAZETI YETU LEO,WAUZA UNGA KUTAJWA BUNGENI HAAAAA KAZI HIPO POLISI,MAHAKAMA NIPO CHALINZE SIJUI NIENDE WAPI?

Sunday 25 August 2013

MUGABE NA ZIMBABWE LEO TENA ANAIBUKA NA KUZISEMA USA NA UK KWA KUUSHAMBULIA UTAWALA WAKE.MPINZANI WAKE ALIISHA FUTA KESI,SASA NI KWA WANANCHI KUFANYA KAZI NA KUENDELEA NA KUSUBILI TENA UCHAGUZI UJAO

Mugabe akiwa wahutubia wananchi wake.
Mugabe na Fidelis Castro.
                                                              Tony Blair na Mugabe.

MATUKIO KATIKA PICHA YA PREMIER LEAGUE UINGEREZA.







VITA,VITA ,VITA SYRIA IPO HATARINI KUSHAMBULIWA NA MAREKANI,UINGEREZA NA UFARANSA BAADA YA KUTUMIA SILAHA ZA SUMU KUWAUA WANANCHI WAKE.

Viongozi wakuu wa kwanza Hollande Francois Ufaransa,Obama Marekani na Waziri mkuu wa Uingereza Cameron wamefanya mazungumzo kwa kutumia njia za simu kuelezea hatua gani wazichukue,lakini uhamuzi mkubwa ni kuishambulia Syria.Mama huyu ni kiongozi wa Ujerumani Mikel Angela.

VITA,VITA NI BAADA YA MAJESHI YA SYRIA KUTUMIA SILAHA ZA SUMU,MAREKANI IMEISHA SOGEZA MELI ZAKE ZA KIVITA BAHARI NA KIONGOZI MMOJA WA JUU WA SERIKALI YA MAREKANI AMESEMA WATAANZA KUTUMIA MAKOMBORA YA MBALI KUHARIBU MIUNDO MBINU YA JESHI LA SYRIA.

 
Rais wa Syria Bashal al Assad. Picha hapo juu ni maiti za waanga walipigwa na bomu la sumu.
Maandamano Syria juu ya silaha za kemikali
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limefanya kikao cha dharura kujadili madai kwamba wanajeshi wa serikali ya Syria wametumia silaha za kemikali pale walipofanya shambulio dhidi ya eneo lililopo nje kidogo ya mji mkuu wa Damascus hapo jana jumatano.
Wanaharakati wa upinzani wamesema kuwa mamia ya watu wakiwemo watoto wameuwawa huku muungano wa upinzani ukiyataja mauaji hayo ya halaiki. Serikali ya Syria imekanusha kwamba imetumia silaha hizo.
Mwenyekiti wa baraza la usalama, Maria Parceval, ambaye ni balozi wa Argentinean katika umoja wa mataifa amesema kuwa wanachama wa baraza hilo wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na madai hayo.
"Naweza kusema kuwa kuna wasiwasi mkubwa miongoni mwa wanachama wa baraza kuhusu madai hayo. Kuna hisia kwamba kuna haja ya kuwa wazi kuhusu kilichotokea na hali kufuatiliwa kwa makini,'' anasema Bi. Maria Parceval.
''Wanachama wote wanakubaliana kwamba matumizi yoyote ya silaha za kemikali, kwa yeyote katika mzozo huu, na katika mazingira yoyote ni ukiukaji wa sheria za kimataifa. Kulikuwa pia na makubaliano ya kutoa wito wa kusitishwa uhasama na vita.''
Kadhalika Bi. Perceval amesema kuwa kulikuwa na makubaliano kuhusu haja ya kuanzisha uchunguzi wa kina kuhusiana na swala hilo.
''Wanachama wa baraza la usalama wametaka katibu mkuu aingilie kati ili kuhakikisha kuwa uchunguzi wa haraka na wa kina usioegemea upande wowote unafanywa. Wanachama wa baraza wameelezea haja ya kutolewa mara moja msaada wa kibinadamu kwa waathiriwa. Hatimaye baraza la usalama limetoa rambi rambi kwa waathiriwa pamoja na familia zao,'' ameongeza kusema Bi. Maria Perceval, mwenyekiti wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Sunday 18 August 2013

MAGAZETI YETU LEO

 

MASHINDANO YA UBINGWA WA DUNIA KWA UPANDE WA MBIO YANAYOFANYIKA URUSI MOSCOW NINAANGALIA TANZANIA WAKIMBIAJI KIMYA HAAAA

Usain Bolt akimaliza mbio za mita 200 akifatiwa na Mjamaika na watatu ni Mmarekani na katika hii picha ni kijana Adam Gemili alishika namba 5 ana miaka 19 na anakimbia vizuri bado techniki hana.

SCOTLAND YARD WAANZA KUCHUNGUZA KIFO CHA PRINCESS DIANA NA DODI KILICHOTOKEA UFARANSA BAADA YA AJALI YA GARI

Princess Diana katika uhai wake alikuwa kipenzi cha watu kutokana na kuwa karibu na jamii.

SERIKALI YA UINGEREZA KUPITIA OFISI YA UHAMIAJI WAWEKA MATANGAZO KWA AJILI YA KUWARUDISHA WAHAMIAJI.BAADA YA MUDA TU WAAANZA KUPATA UPINZANI KUTOKA NJE YA UINGEREZA NA NDANI YA UINGEREZA


ROONEY NA MAN U ANAKAZI KUBWA KURUDI KUWA FIT ILI KUWA KWENYE KIKOSI CHA KWANZA CHA MAN U ANATAKA KUHAMA LAKINI BADO MIPANGO KUKAMILIKA UENDA AKAENDA CHELSEA.


Saturday 3 August 2013

MUGABE NA ZIMBABWE,KIONGOZI WA UPINZANI AKILIA KWA UCHUNGU


Kiongozi wa upinzani akitokwa machozi baada ya Mugabe kupata ushindi ni kiongozi wa upinzani Tsvangalai akilia maana alikuwa ni waziri mkuu sasa anakaa benchi.









Friday 2 August 2013

MICHEZO BILA WATOTO AU VIJANA HATUNA TIMU HII NI BAKET BALL ENZI HIZO HII TIMU BAADAYE ILIWEZA KUCHUKUA KOMBE LA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Mpira au mchezo wowote unaanza kwa watoto aAmina Ahmed Hili chama lilikua bonge la chama aisee...tulikua tunaingia uwanjani na ngoma,wengine hadi tulikua tukirudi hme unakuta umesubiriwa mlangon maana tulikua tukiomba ruhusa tukanyimwa bac tulikua tunatoroka,lolu vijana tunavyosema.Hii ilikuwa ni timu ya chini ya miaka 18 chini ya kocha Del ambaye baadaye ilikuja kuchukua komba la Afrika mashariki na kati basket ball.kuna mchezaji mmoja nimechukua Facebook

UK UHAMIAJI YAANZA KUPIGWA VITA BAADA YA KUANZISHA OPERASION KAMATA KAMATA WAAMIAJI KWA KUWAKAMATA WATU WAKIWA NJIANI.


Uingereza katika sakata la kukamata Waamiaji lakisha watu waanza kupinga Rais wa Nigeria naye azungumzia sakata hilo.Wananchi waanza kupinga na kusema ni Ubaguzi wa Waafrika.

JKT MPYA HIYO HAYA HAKI SAWA HAKUNA UNYASAJI HAPO.

Vijana wetu waliopitia JKT wakiwa katika picha yao baada ya mafunzo yao wakiwa katika Pozi lao ongereni wakina dada.

SIMBA NA YANGA WACHEZAJI WA AFRIKA MASHARIKI NDIO GUMZO LAKE,KWA NINI WASIWAANGALIE WA AFRIKA YA MAGHARIBI?



Mabeki wa wawili wa kimataifa kutoka Burundi na Uganda wamewasili nchini leo tayari kwa ajili ya kukamilisha usajili wao na Wekundu wa msimbazi Simba msimu huu.
Afisa habari wa timu hiyo Ezekiel Kamwaga amesema kuwa beki wa kati Joseph Owino aliwasili nchini asubuhi ya leo na jioni hii amewasili beki Girbert Kazi kutoka burundi
kwa upande mwingine Kamwaga amesema kuwa taarifa za kusajiliwa na Yanga kwa kiungo mwenye kasi raia wa Uganda anayecheza soka nchini Vietnam Moses Oloya si za kweli kwani mchezaji mwenyewe amewahakikishia atatua katika timu hiyo
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUPATA HABARI ZILIZOPITA BONYEZA OLDER POSTS