KARIBU SANA TOSA MAWE BLOG KWA HABARI MBALIMBALI TOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA PIA TUTUMIE HABARI MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +447896103988 +447438590583 | E-mail: mwamfilingef@gmail.com NYOTE MNAKARIBISHWA SANA ASANTENI . | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US CLICK HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Monday 26 August 2013

TANZANIA NCHI YETU INAPOCHEZEA BANDARI,SASA UGANDA NA RWANDA KUACHA KUTUMIA DAR PORT,WAZIRI WETU WA UCHUKUZI ANASEMA NI MWENDA WAZIMA ATAKAYEACHA KUTUMIA BANDARI YA DAR KWANI NI KARIBU UKITUMIA KENYA NI MBALI KWELI ATA KAMA KUNA MATATIZO WATUMIE TU KWELI TUPO PABAYA TUSUBIRI MADHARA YAKE YA AJIRA NA MAPATO,TUSUBIRI TENA CONGO,ZAMBIA NA MALAWI NAO WALIISHA SEMA WATATUMIA MSUMBIJI AU AFRIKA YA KUSINI

Dar es Salaam. Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania (Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.
Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini Serikali haikuchukua hatua.
Hanspope alisema ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ni baadhi ya vikwazo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara mbalimbali wa nchi hizo.
“Serikali ipunguze gharama za ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ili kuwa na ushindani sawa na bandari nyingine na hivyo kuzivutia kutumia Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Hanspope.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo alikataa kuzungumzia lolote kuhusu suala hilo akisema halina mantiki yoyote kwake.... “Hivi hilo jambo unaloniuliza lina sense (mantiki) yoyote? Mie siwezi kujibu lolote nenda ukamuulize mwenyewe (Hanspope) maana wakati akisema mimi sikuwepo.”
Alisema kujitoa kwa Rwanda na Uganda kuitumia Bandari ya Dar es Salaam hakutakiathiri chama hicho tu, bali uchumi wa taifa kwa ujumla.
Hayo yanatokea wakati Rwanda ikiendeleza vita yake ya maneno na Tanzania na mfululizo wa matukio ya kuitenga Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Viongozi wa Kenya, Rwanda na Uganda walikutana Juni 25, mwaka huu mjini Entebbe, Uganda na kukubaliana kuongeza uhusiano wa kibiashara baina yao.
Kamati ya Bajeti
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge alisema katika kikao kijacho cha Bunge, kamati hiyo itaibana Serikali kuhusu mikakati inayofanywa kukabiliana na ushindani wa kibiashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Alisema sababu ya Rwanda na Uganda kujitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam ni vikwazo katika barabara ikiwamo mizani mingi ya kupimia mizigo.
“Mizani ni mingi pia kuna usumbufu katika kupima mizigo yao na kwamba hali hiyo inawaletea usumbufu wafanyabiashara wengi,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUPATA HABARI ZILIZOPITA BONYEZA OLDER POSTS