KARIBU SANA TOSA MAWE BLOG KWA HABARI MBALIMBALI TOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA PIA TUTUMIE HABARI MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +447896103988 +447438590583 | E-mail: mwamfilingef@gmail.com NYOTE MNAKARIBISHWA SANA ASANTENI . | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US CLICK HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Sunday 30 December 2012

INDIA NCHI YENYE UVUNJAJI WA SHERIA KAMA AFRIKA AU NCHI ZA DUNIA YA TATU

 
ALIYEBAKWA AZIKWA INDIA.FUJO ZIPO PALE WANANCHI WAANDAMANA.
 
India nchi ambayo inasifika kwa kutoa wataalamu wa sheria lakini nchi hii imegubikwa na vitendo vya rushwa mpaka inatishia amani.
Nilienda kwenye duka la Asian ndio Wahindi na nilikuwa natafuta vitabu vya mtoto kuongea nao wakanionyesha vitabu,wakaniambia angalia kwenye kabati nikaangalia na kukuta vitabu vya Polisi na matatizo ya Rushwa nilishangaa sana lakini nikakumbuka zile sinema za Amitha Banchan wakionyesha Polisi wanavyopewa Rushwa na majambazi.
Tatizo la Ubakaji kwa vijana wa Kike limewaingiza katika tatizo kubwa la uvunjaji wa amani. India nchi yenye kesi nyingi za ubakaji lakini hazina hukumu.
 
 

GEORGE BUSH MKUBWA NA GEORGE BUSH MTOTO

George Bush Snr amepata nafuu ana miaka 88,Madaktari na manesi wanashirikiana naye kuimba sasa maana anafuraha sasa baada ya kupata nafuu.

MAGAZETI YETU LEO






Saturday 29 December 2012

SOKO LA BAHARINI UKIWA MTEJA NI LAZIMA UWEZE KURUKIA MTUMBWI MMOJA BAADA YA MWINGINE KUFUATA BIDHAA NI THAILAND


WACHEZAJI WA TIMU YA FIFA WALIPOPAMBANA NA TIMU YA BRAZIL WAZEE(VETERAN) NA VIJANA

 Mchezo wa hisani wa kuchangia maskini uliochezwa Brazil,ulichezeshwa na refa mstaafu Collin.
 
Zidane na Deco wakimkaba Ronaldo ambaye ana kakitambi,Zidane alimchezea rafu.
 
Zidane akizozana na Ronaldo wewe uniwezi mimi niko fit cheki wewe una kakitambi na katikati ni Neymar anayetegemewa kuhamia Man City msimu huu Januari ni mchezaji hodari kwa sasa Brazil.
 
Hooo Zico naye wamo anakimbiza mpira enzi zake mpira hauzeeki ila mwili.
 
 

UBUNIFU NI UJANJA WAKO WEWE KUPAMBA KUTOKANA NA MAZINGIRA YAKO


PANADOL NA HASARA ZA KUTUMIA -UJUMBE KUTOKA KWA KHERI CHALAMILA ,MUFINDI



 
Mume wangu alikuwa akifanya kazi katika hospitali kama mhandisi IT, kama hospitali ni mipango ya kuanzisha database ya wagonjwa wake na yeye anajua baadhi ya madaktari vizuri kabisa. madaktari kutumika kumwambia kuwa wakati wowote kuwa na maumivu ya kichwa, wao si tayari kuchukua panadol / PARACETAMOL.
Kwa kweli, wao kurejea kwa dawa za mitishamba au kupata njia nyingine. Hii ni kwa sababu panadol ni sumu kwa mwili, na hivyo inaleta madhara ya ini. Kulingana na daktari, panadol kubaki katika mwili kwa angalau miaka 5. 

Monday 24 December 2012

HERI YA KRISTMAS KWA WANAJAMII WOTE MUNGU AWABARIKI WOTE.


MAGAZETI YETU LEO SIJUI LINALOSEMA UKWELI NI LIPI KATI YA HAYO MAGAZETI




WAMEISHA KUWA WAZEE KUCHEZA MPIRA LAKINI BADO WAMO,UNAWEZA KUWAKUMBUKA?


VIDUKU AU KIDUKU,UCHEZAJI HUU INABIDI UWE FIT LAA O UNTOA MACHO AU KICHWA KWA KHUKU UKIANGALIA CHINI


MAGAZETI YANAYOPENDWA NA WENGI KWA STORI ZA MITAANI





CHRISTMAS NI SHEREHE INAYOSHEREKEWA KWA KULA CHAKULA CHA CHRISTMAS YAANI BATA MZINGA,VIAZI MVIRINGO,KAROTI,VIKABICHI VYA MVIRINGO,GRAVI, PUDDING NA CREAM AU CUSTARD

Sherehe yoyote ni mlo na vinywaji kama vile Pilau,wali wa maji na kuku hivyo ndio vyakula vyetu,ukienda nchi zingine nao wanachakula wanasema vya jadi na ni lazima viwepo ili  sherehe ifanyike kama Watu wa Ulaya ni lazima kuwa na Bata mzinga.Picha hiyo hapo juu ni chakula cha Christmas kwa wenzetu Waingereza. 

Tuesday 18 December 2012

CHRISTMAS MAFATHER CHRISTMAS WAKIWA KATIKA MAONYESHO


MCHEZAJI GOLFU MAARUFU ALIYESHIKILIA NAMBA MOJA SASA AMEISHA SHUKA KIWANGO TIGER WOOD.


Tiger Wood hatakiwa kushiriki Australia Golf kwa sababu tajiri wa Hotel na uwanja wa Golf Bilionea Clive Palmer amesema hayupo tena kwenye Chart kwa hiyo Hasishiriki,hapo hukute waliisha liwa kamari.

BAADA YA AJALI MBAYA BWANA HARUSI AFUNGA NDOA MBEYA


  1.  Bwana harusi Emmanuel Mwangosi na Bibi harusi Magreth Ntebe wakiwa na furha ya huzuni lakini ndoa ilikwisha fungwa,Mungu apewe sifa maana Bwana harusi alipata Ajali mbaya bahati nzuri aliumia.Tunampa pole na maisha mema ya ndoa.
Ajali ambayo iliyompata bwana Emmanuel Mwangosi,watu hawakujua jamaa kapona lakini Mungu ni mkubwa jamaa aliumia na kisha kufunga ndoa yake kanisani na majeruhi.
Picha na Mbeya yetu Blog.

Sunday 16 December 2012

CHELSEA YAKOSA TENA UBINGWA WA KLABU BINGWA WA DUNIA NCHINI JAPAN

Golikipa wa Corinthians akimwambia Torres uwezi kitu mie natoka Brazil.

 Oscar wa Chelsea akipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya mchezaji wa Corinthians.
Wachezaji wa Coriantians wakisherekea ushindi wa Ubingwa wa dunia.



JESHI LA POLISI LINA WAKATI MGUMU KWA SASA NI LAZIMA VIONGOZI WETU WAJADILI MATATIZO YA UGOMVI KATI YA POLISI NA RAIA

Polisi wawili wauawa Ngara

undefined
IGP Said Mwema.
Kwa ufupi
“Wananchi walimvamia yule askari aliyebaki pale gereji na kuanza kumkata kwa mapanga na kumpiga mawe hadi akafariki dunia,” alisema.
WANANCHI wa Kata ya Mugoma, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera wamewaua askari polisi wawili na kuchoma moto Kituo cha Polisi Mugoma kwa madai kuwa polisi hao wamemuua kwa kumpiga risasi mwananchi mwenzao bila hatia.
Tukio hilo la lilitokea jana mchana wilayani humo na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi.
Akizungumza wakati akielekea eneo la tukio, Kamanda Kalangi alisema: “Tukio limetokea Kijiji cha Mugoma, sina details (maelezo ya kina), kwa sababu ndiyo nakwenda huko, ila nikifika ndipo nitajua nini kimetokea, nitatoa maelezo kwa kina.”
Habari zilizorushwa na Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC), jana jioni zilieleza kuwa askari polisi waliouawa ni Koplo Pascal na Konstebo Alex wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilayani Ngara.
Katika taarifa hiyo ya BBC, Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Costa Kanyasu naye alithibitisha vifo vya askari hao na kueleza kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi kujua ukweli wa tukio hilo, ikiwa ni pamoja na kujua kama askari hao ndiyo walimpiga risasi mwananchi huyo.
Ilidaiwa kuwa polisi hao walifika katika Kijiji cha Mugoma kwa lengo la kukagua pikipiki mbovu na zisizokuwa na usajili.
Walipokuwa katika ukaguzi huo walifika katika gereji moja na kukuta mmiliki wake akitengeneza pikipiki, wakamtaka aipeleke kituoni kwa maelezo kuwa ilikuwa mbovu.
Ilidaiwa kuwa fundi huyo aligoma kutekeleza amri hiyo na katika ubishi, polisi mmoja alimpiga risasi na kufariki dunia papohapo.
Kitendo hicho kiliamsha hasira kwa wananchi waliokuwa jirani na eneo hilo ambao walianza kujikusanya katika eneo la tukio.
Mmoja wa watu mashuhuda wa tukio hilo, Mwandishi wa Habari wa Redio Kwizera iliyopo wilayani Ngara, Joyce Ngalawa alisema kuona hivyo, polisi anayedaiwa kufyatua risasi alikimbia na kujificha katika nyumba iliyopo jirani na gereji hiyo, huku akimwacha mwenzake.
“Wananchi walimvamia yule askari aliyebaki pale gereji na kuanza kumkata kwa mapanga na kumpiga mawe hadi akafariki dunia,” alisema.
Alisema baada ya mauaji hayo, wananchi hao walikwenda katika nyumba aliyokuwa amejificha askari wa pili na kutishia kuichoma moto iwapo angegoma kutoka.
“Mmiliki wa nyumba ile baada ya kuona wananchi hao wanataka kuichoma moto nyumba yake, alimtaka askari huyo atoke nje. Alipotoka tu, wananchi walimvamia na kuanza kumpiga mawe na kumuua,” alisema.

 


 

 
Sharing this page …
Thanks! Close

Showing 4 comments

  • Hamadi Marwa 1 comment collapsed CollapseExpand
    Askari waache ubabe wa kutoa hukumu ya kifo na kuitekeleza kwa raia wasio na hatia. Polisi wanatakiwa kufanya kazi kisayansi zaidi na ndio maana taaluma ya saikolojia na sosholojia ni ya muhimu sana kwa walinzi hawa wa usalama wa raia na mali zao. Kazi kwako IGP maana wananchi sasa wamechoka na watu waliochoka hawana subira sijui mahakama au utwala wa sheria!!!!!
     
     
  • Lupaya 1 comment collapsed CollapseExpand
    I weje iwe haki kwa wananchi kuuawa na polisi na i we haramu kwa wao polisi kufanyiwa hivo hivo na wananchi? Mie nasema dawa ya moto ni moto, na kumwogopa mwonezi kunamwongezea nguvu ya kukuonea. Wananchi hawana njia nyingine sasa. Kama ni uvumilivu wamevumilia mengi na kwa muda mrefu     
  • Kadogoo 1 comment collapsed CollapseExpand
    Kila wananchi wakiua mtu wanapewa jina la "wenye hasira kali". Nadhani waandishi wa habari wanachochea tabia hii. Habari hiyo hiyo inalaani wananchi "kujichukulia sheria mkononi" na hiyo hiyo inawalinda "wenye hasira kali". Tujifunze kupamba matukio.
        
  • semakweli2012 1 comment collapsed CollapseExpand
    Mimi ninavyoona kuna mapungufu makubwa katika uteuzi, mafunzo na hata usimamizi mzima katika jeshi la polisi. Sasa jeshi la polisi halina tofauti na majambazi, ukimuona polisi anakuja unalazimika kukimbia hata kama huna kosa manaa akikufika anaweza tu kuamua kukupiga risasi na isiwe chochote, bosi wake akatoa maelezo ilikuwa bahati mbaya.
    Hichi kipindi cha karibuni tumeshuhudia mauaji ya watu mbali mbali yanayofanywa na polisi wakiwemo waandishi wa habari, raia wa kawaida, wafuasi wa vyama vya upinzani na sasa hata kwa wajasiriamali (fundi gereji).
    Kama wanavyotumia wenyewe hiyo waliofanya wananchi ni kujihami (Self Defence), wewe polisi kwa jeuri unampiga risasi raia kwa sababu tu kakataa amri yako.
    Kwa kweli tunahitaji mabadiliko makubwa katika jeshi letu la polisi kuanzia juu mpaka chini ili lirejeshe imani na hadhi yake kwa jamii.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUPATA HABARI ZILIZOPITA BONYEZA OLDER POSTS