KARIBU SANA TOSA MAWE BLOG KWA HABARI MBALIMBALI TOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA PIA TUTUMIE HABARI MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +447896103988 +447438590583 | E-mail: mwamfilingef@gmail.com NYOTE MNAKARIBISHWA SANA ASANTENI . | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US CLICK HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Sunday 25 August 2013

VITA,VITA NI BAADA YA MAJESHI YA SYRIA KUTUMIA SILAHA ZA SUMU,MAREKANI IMEISHA SOGEZA MELI ZAKE ZA KIVITA BAHARI NA KIONGOZI MMOJA WA JUU WA SERIKALI YA MAREKANI AMESEMA WATAANZA KUTUMIA MAKOMBORA YA MBALI KUHARIBU MIUNDO MBINU YA JESHI LA SYRIA.

 
Rais wa Syria Bashal al Assad. Picha hapo juu ni maiti za waanga walipigwa na bomu la sumu.
Maandamano Syria juu ya silaha za kemikali
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limefanya kikao cha dharura kujadili madai kwamba wanajeshi wa serikali ya Syria wametumia silaha za kemikali pale walipofanya shambulio dhidi ya eneo lililopo nje kidogo ya mji mkuu wa Damascus hapo jana jumatano.
Wanaharakati wa upinzani wamesema kuwa mamia ya watu wakiwemo watoto wameuwawa huku muungano wa upinzani ukiyataja mauaji hayo ya halaiki. Serikali ya Syria imekanusha kwamba imetumia silaha hizo.
Mwenyekiti wa baraza la usalama, Maria Parceval, ambaye ni balozi wa Argentinean katika umoja wa mataifa amesema kuwa wanachama wa baraza hilo wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na madai hayo.
"Naweza kusema kuwa kuna wasiwasi mkubwa miongoni mwa wanachama wa baraza kuhusu madai hayo. Kuna hisia kwamba kuna haja ya kuwa wazi kuhusu kilichotokea na hali kufuatiliwa kwa makini,'' anasema Bi. Maria Parceval.
''Wanachama wote wanakubaliana kwamba matumizi yoyote ya silaha za kemikali, kwa yeyote katika mzozo huu, na katika mazingira yoyote ni ukiukaji wa sheria za kimataifa. Kulikuwa pia na makubaliano ya kutoa wito wa kusitishwa uhasama na vita.''
Kadhalika Bi. Perceval amesema kuwa kulikuwa na makubaliano kuhusu haja ya kuanzisha uchunguzi wa kina kuhusiana na swala hilo.
''Wanachama wa baraza la usalama wametaka katibu mkuu aingilie kati ili kuhakikisha kuwa uchunguzi wa haraka na wa kina usioegemea upande wowote unafanywa. Wanachama wa baraza wameelezea haja ya kutolewa mara moja msaada wa kibinadamu kwa waathiriwa. Hatimaye baraza la usalama limetoa rambi rambi kwa waathiriwa pamoja na familia zao,'' ameongeza kusema Bi. Maria Perceval, mwenyekiti wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUPATA HABARI ZILIZOPITA BONYEZA OLDER POSTS