KARIBU SANA TOSA MAWE BLOG KWA HABARI MBALIMBALI TOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA PIA TUTUMIE HABARI MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +447896103988 +447438590583 | E-mail: mwamfilingef@gmail.com NYOTE MNAKARIBISHWA SANA ASANTENI . | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US CLICK HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Friday 24 July 2020

KAMPENI ZA RUSHWA TANZANIA KWA AJILI YA UCHAGUZI WA KUTEUA WABUNGE KATIKA KURA ZA MAONI NI SAWA NA KUMPIGIA MBUZI GITAA

  CCM ni kazi kubwa sana kuweza kuzuia Rushwa.Watia nia wanatumia sana pesa kuwarubuni wajumbe au Wajumbe wanaomba Rushwa kusema kwamba Mkuu hatujala au mkuu unatuachaje?Au tupe chetu ukipata Ubunge uwezi kutukumbuka ndio chanzo cha kugawana Rushwa kinavyotokea.
Suala lingine ni Mameneja au watu wanaomwakilisha mtia nia kwa kuweza kuwashika wajumbe na huyo anayemwakilisha mgombea fulani yeye ndiye mshika pesa za huyo mtia nia na wajumbe kumfuata na kupata kitu kidogo hiyo ni kazi kuwakamata hawa watoa Rushwa.Nilikuwa na jamaa wakati wa uchaguzi wa kura za kumteua mgombea ubunge watu walikuwa wakitoka Dar es salaam kwenda mikoani kumfanyia kampeni mgombea aliyejipanga kupata Ubunge kupitia CCM sasa tujiulize kwa nini iwe hivyo?je huyo aliyechaguliwa kwa rushwa atakuwa kiongozi anayejali maslahi yako au maslahi yake?Kwa hali hiyo tunaomba Mwenyekiti wa taifa CCM na wajumbe wake wapitie hii hali na kuibadilisha CCM kuanzia mashinani ili kuboresha maendeleo ya chama.Kuna habari Mwenyekiti fulani anasaidia mjumbe fulani ili awe mbunge na wananchi wamekuja juu na kulalamika hiyo ndio hali tulionayo ya Rushwa kwa nini awe anasaidia mtu fulani?kazi ipo kwa kuweza kubadilisha CCM ambayo ina wajumbe Wapiga deal na kwa sababu uchaguzi kila baada ya miaka mitano basi tunasahau.Muhimu ni kwa chama kurekebisha haya matatizo yasije kutokea tena.
Tosamawe





No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUPATA HABARI ZILIZOPITA BONYEZA OLDER POSTS