KARIBU SANA TOSA MAWE BLOG KWA HABARI MBALIMBALI TOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA PIA TUTUMIE HABARI MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +447896103988 +447438590583 | E-mail: mwamfilingef@gmail.com NYOTE MNAKARIBISHWA SANA ASANTENI . | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US CLICK HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Tuesday 31 March 2015

ASKOFU GWAJIMA- MAASKOFU MBALIMBALI KUTINGA KWA IGP KUMWOMBEA MSAMAHA ASKOFU GWAJIMA,LAKINI SHERIA INABANA TUIACHE SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE


 MAASKOFU WAKIINGIA UKUMBINI KWA AJILI YA KUTOA TAARIFA YA KUMWOMBEA MSAMAHA ASKOFU GWAJIMA



 MAASKOFU wa makanisa mbalimbali ya Kipentekoste nchini wamesema wanatarajia kwenda kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu ili kulimaliza sakata la Askofu Josephat Gwajima, kwani kuliendeleza ni kuleta mpasuko wa kidini katika jamii.


Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Maaskofu hao, Askofu Dk. Damas Mukassa alisema hakuna sababu ya jambo hilo kukuzwa, kwani mhusika amemsamehe Askofu Gwajima.

Dk. Mukassa alisema ni vema Serikali na vyombo vya usalama vikatumia weledi katika kushughulikia mambo ya kidini na viongozi, kwani yanaweza kusababisha chuki baina yao.

"Tunaomba Serikali isaidie kuondoa mkanganyiko huu, na busara itumike ili kuepusha uvunjifu wa amani katika jamii," alisema Mukassa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUPATA HABARI ZILIZOPITA BONYEZA OLDER POSTS