KARIBU SANA TOSA MAWE BLOG KWA HABARI MBALIMBALI TOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA PIA TUTUMIE HABARI MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +447896103988 +447438590583 | E-mail: mwamfilingef@gmail.com NYOTE MNAKARIBISHWA SANA ASANTENI . | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US CLICK HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Wednesday 11 March 2015

ALBINO WANAVYOTESEKA SASA SERIKALI NI VITA NA WATU WOTE WANAHUSIKA NA BIASHARA HIYO HARAMU.

 VITA KATI YA WAGANGA WA JADI WACHAWI NA SERIKALI NANI ATASHINDA?
KILA AKIPOTEA ALBINO WAGANGA NA WANAJIHUSISA NA BIASHARA YA VIUNGO HIVYO VYA ALBINO WAPELEKWE JERA.
POLISI mkoani Rukwa wanawashikilia watu 15, wakiwemo waganga wa kienyeji saba kwa tuhuma za kuhusika kwenye tukio la kukatwa kiganja cha mtoto Baraka Cosmas.
Baraka (6), ambaye ni mlemavu wa ngozi, alikatawa kiganja cha mkono mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akiwa amelala na mama yake usiku.
Watuhumiwa hao walitiwa mbaroni kufuatia msako mkali unaoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani hapa, ikiwa ni muda mfupi baada ya tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, alisema kikosi maalumu cha polisi kinaendelea na msako mkali kuhakikisha mtandao wote wa utekaji na mauaji ya albino unatiwa mbaroni.
Alisema baada ya kutiwa mbaroni watuhumiwa hao, walianza kutajana hadi kufikia 15, ambao wote kwa sasa wanaendelea kuhojiwa kabla ya kupandishwa kizimbani kujibu mashitaka yanayowakabili.
Kamanda Mwaruwanda aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Mwendesha William (30), Masunga Bakari (50), David Kiyenze (45) na Ngolo Masinga (47), wote wakazi wa Kijiji cha Kaoze wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.
Wengine ni Mageta Shimba (46), Pascal Jason (40), Mnyika Managa pamoja na baba mzazi wa Baraka, Cosmas Yolam (32).
Waganga wanaoshikiliwa ni Eliza Malongo (36), Sodeli Malimbo, maarufu kama Chuchi (66), Akobo Chinzwe (50), Leonard Samson (59) na Inglibert Kasinde (45).
Wengine ni Boniphace Chalya (49), Charles Misalaba (47) na Julius Simbamwene (40).
Alisema waganga wa jadi hao walikutwa na vifaa vya kuagua na kupigia ramli pamoja na nyara za serikali kama vile mayai ya mbuni, kucha za chui, ngozi ya pakapori, kobe aliyekaushwa, ngozi ya chui na nywele zinazosadikiwa ni za binadamu
Mama wa mtoto aliyekatwa kiungo aliumizwa naye.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUPATA HABARI ZILIZOPITA BONYEZA OLDER POSTS