KARIBU SANA TOSA MAWE BLOG KWA HABARI MBALIMBALI TOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA PIA TUTUMIE HABARI MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +447896103988 +447438590583 | E-mail: mwamfilingef@gmail.com NYOTE MNAKARIBISHWA SANA ASANTENI . | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US CLICK HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Sunday 21 July 2013

MUUNGANO ULIISHA KWISHA KUFA SIKU NYINGI KISHERIA,ILA KWA SABABU TULIO WENGI HATUJUI SHERIA AU KATIBA BASI MUUNGANO UPO.NI KOSA KUONGOZA KWA KUTOKUFUATA KATIBA YA MUUNGANO MUHIMU KUWA NA SERIKALI TATU.

Tundu Lissu Akizungumza katika Kipindi cha Makutano na Fina Mango
Mbunge wa Singida Mashariki, Mheshimiwa Tundu Lissu amesema Muungano wa Tanzania umekufa kikatiba. Lissu aliyasema hayo wakati alipoulizwa msimamo wake juu ya rasimu ya katiba na muundo wa serikali katika kipindi cha Makutano kinachoendeshwa na Fina Mango, Magic FM.

Akijibu swali hilo alitolea mfano wa wakati wa maadhimisho ya siku ya mapinduzi ya Zanzibar ambayo alisema anaekagua gwaride na kupigiwa mizinga 21 anatakiwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye amiri jeshi mkuu lakini kwa sasa katika maadhimisho hayo rais wa Zanzibar ndiye anayefanyiwa yote hayo kutokana na katiba ya sasa ya Zanzibar kuitambua Zanzibar kama nchi.

Alisema "Katiba ya sasa ya Zanzibar inasema rais wa Zanzibar ni mkuu wa nchi ya Zanzibar, ni kiongozi wa serikali, ni Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Idara Maalum. Kimsingi sababu kubwa ya Muungano ilikuwa ni  masuala ya ulinzi na usalama na Zanzibar imeyaondoa kwenye Muungano" na kumalizia kusema kuwa katiba ya sasa ya Zanzibar ya leo ni waraka wa Uhuru.

Lissu alimalizia kwa kusema namna pekee ya kubaki na Muungano ni kuwa na serikali tatu huku akiwakosoa wanaosema mapendekezo ya tume ya katiba kuwa serikali tatu ni gharama wanakosea kwani hakutakuwa na gharama kubwa kwa kusema kutakuwa na jumla ya wabunge 314  tu tofauti na sasa ambapo kuna jumla ya wabunge 438 tu.

Hata hivyo alipoulizwa kama CHADEMA inaona kuna haja kuwepo Muungano alisema ipo na kuongezea "Ndoa ya kulazimishana hapana, kama upande mmoja unataka out is out". Lissu alimalizia kwa kusema wananchi wa kawaida wa Zanzibar hawautaki Muungano kwani hawaoni faida yoyote. 


 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUPATA HABARI ZILIZOPITA BONYEZA OLDER POSTS