KARIBU SANA TOSA MAWE BLOG KWA HABARI MBALIMBALI TOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA PIA TUTUMIE HABARI MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +447896103988 +447438590583 | E-mail: mwamfilingef@gmail.com NYOTE MNAKARIBISHWA SANA ASANTENI . | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US CLICK HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Tuesday 4 January 2022

UPINZANI TANZANIA BADO HAUNA TIJA KWA WANANCHI-MFANO MWENYEKITI WA NCCR MAGEUZI KUMSIFIA SPIKA KAONGEA VEMA NI KOSA KWA UPINZANI KUMTETEA MTU ALIYEONGELEA MAMBO MAGUMU KWA NCHI SEHEMU HISIYO MAALUM WAKATI YEYE NI SPIKA ANA MAMLAKA YA KUONGEALEA BUNGENI

Leo ngoja tuongelee Upinzani husio kuwa makini na Maslahi ya wananchi Mwenyekiti Mbatia kuongea mbele ya umma kwa kusema Mh Spika kafanya vizuri kuongea nchi inakopa sana hiyo sio siasa ya vyama vingi na ni kosa kwa kiongozi kama Mbatia kusema hayo.Rais kaongea vema kuliko Mwenyekiti Mbatia Sasa Tuanze na makosa mengi yanayofanywa na Upinzani ikiwepo suala la kuwaeleza Wananchi ni jinsi gani Serikali iliyopo madarakani inavyotumia pesa za umma na matumizi makubwa ya pesa za serikali. Kuwa na viongozi kama Wakuu wa Mikoa Wakuu wa Wilaya ambao hawahitajiki kwenye uongozi maana tuna Mameya na tuna wakurugenzi leo hii Mwenyekiti Mbatia anamsifia Spika kaongea vema. Upinzani hauongeleei Uchumi kwa nini wafanyakaz hawapandishwi mishahara miaka sita sasa na kwa nini huduma za Afya zipo duni na Elimu ipo hivyo hivyo wao kama Upinzani watafanya nini ili kuwapa wananchi maisha bora sio wangjee kampeni na kuongea kuhusu Spika hasiye kuwa na uwezo wa kuongoza wabunge. Wananchi wanahitaji Elimu nzuri ya matumiziya pesa zao za kodi nani anawasemea ni upinzani lakini upinzani wetu hawana habari ya Uchumi wetu na matumizi ya serikali. Ukija kwenye Afya hospital zetu zipokwenye hali duni ya kukosa vifaa tuna majengo na vifaa hakuna na serikali ya CCM wanajisifia wapo vizuri kwenye huduma za Hospital nyingi za mikoani hawana mashine ya CT Scanner kwa kutumia kupiga picha za ndani ya mwili X ray upinzani hawana habari.Je nani atawasemea wananchi ni upinzani kuwaelezea wananchi nao wafahamu ili waweze kuwachagua. Wapinzani kutumia Ruzuku kwa kutokuendeleza chama mfano kuna vyama vilikuwa na wabunge wengi na Ruzuku kubwa lakini hata kujenga ofisi ya Chama hawana sasa imani kwa wannachi itatoka wapi. Upinzani Tanzania ni lazima kubadilika sasa na kuwaelimisha wananchi kila leo kuhusu serikali ilikwama na wao watafanya nini Kazi kwenu Upinzani kama unataka kuongoza nchi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUPATA HABARI ZILIZOPITA BONYEZA OLDER POSTS