KARIBU SANA TOSA MAWE BLOG KWA HABARI MBALIMBALI TOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA PIA TUTUMIE HABARI MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +447896103988 +447438590583 | E-mail: mwamfilingef@gmail.com NYOTE MNAKARIBISHWA SANA ASANTENI . | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US CLICK HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Thursday 11 December 2014

WAZIRI HAKANA KUCHANGIA ELFU 15,000 KWELI HAIWEZEKANI KWA WAZIRI ANALIPWA PESA NYINGI KUCHANGIA ELFU 15.HIZO NI SIASA CHAFU


Aidha, Mheshimiwa waziri wangu Chana ambae ndiye Wizara yake inahusika na watoto, kwa kuliona tatizo hilo la vyumba vya madarasa kuezuliwa alionyesha kuguswa zaidi na hata kuwa kiongozi wa kwanza kuanza kuchangia mchango kwa ajili ya harambee ya ujenzi wa vyumba hivyo kwa kuchangia kiasi cha Tsh 15,000/= kupitia kwa mkuu wa shule hiyo Agnes Mageza ambaye pia kulingana na utaratibu wa ukusanyaji wa fedha hizo na kuepuka matumizi yasiyotarajiwa na fedha za maafa,  alilazimika kuzipeleka fedha hizo kwa Afisa Mtendaji wa kijiji ili kuzihifadhi kwa taratibu na kutoa stakabadhi kwa kila mchangiaji kama ilivyo taratibu za upokeaji wa fedha za michago mbalimbali.


Pamoja na Waziri Pindi, Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe katika kuunga mkono jitihada za wapiga kura wake kwa wakati huo alipeleka saruji mifuko 50 ili kuanza kukarabati shule hiyo huku wananchi wakichangishana kiasi cha Tsh milioni 1.8 kati ya zaidi ya Tsh milioni 13 zilizokuwa zikihitajika ili kurejesha vyumba hivyo vya madarasa katika hali yake na watoto wapata kusoma.

Kasi ya michango kwa wananchi ilikuwa chini zaidi kwani hadi Desemba hii ni Tsh milioni 1.8 pekee na saruji mifuko 50 ndio iliyopatikana na kama kasi hiyo ingeendelea,  hivyo hadi wananchi hao waweze kujenga vyumba hivyo kwa kupata Tsh milioni 13 basi ingekuwa ni mwakani mwezi Desemba.

Kwa kuliona hilo na uchungu wa maendeleo ya elimu kwa watoto hao mbunge Filikunjombe alilazimika kujitolea kujenga upya vyumba hivyo kwa zaidi ya Tsh milioni 13 ujenzi ulioanza Jumatatu wiki hii na wakati wa kujitolea  kufanya hivyo Mkuu wa Shule hiyo, Bi Mageza na Katibu Tarafa ya Mawengi waliwashukuru wadau mbalimbali waliochangia akiwemo Waziri Chana aliyechagia Tsh 15,000.

Ajabu ni kwamba, baada ya vyombo vya habari kuripoti habari hiyo ya Waziri kupongezwa kwa kuchangia kiasi hicho cha fedha, Waziri Chana alinukuliwa akikana kuchangia maafa katika shule hiyo na hata kudai kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanamchafua

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUPATA HABARI ZILIZOPITA BONYEZA OLDER POSTS