Kutokana na janga kubwa lililozikumba nchi nyingi duniani ni kwamba sasa Uchumi unazidi kudidimia asa kwa zile nchi zinazotegemea misaada kutoka nje yaani nchi za dunia ya tatu.
Tukija kwenye uchumi wa nchi zilizoendelea wao wana mbinu nyingi za kuwasaidia watu wao kwa kuwapa msaada wa mikopo na pesa za kujikimu sasa kwa nchi za dunia ya tatu watu wanajiendesha wenyewe.
Utalii unazidi kudidimia kwa kasi kwa sababu Watalii wananogopa kusafiri na Oda zote zilizokwisha lipwa kwa ajili ya Utalii kwa mfano serikali ya \uingereza imewaambia Mawakala wa utalii kuwarudishia wateja wao pesa.Hii ni pigo kbwa kwa utalii kwa nchi nyingi zikiwemo za Afrika Asia na Amerika kusini.
Utalii wa kutumia Meli umeisha punguza wafanyakazi 200,000 ili kwendana na wakati kukiwa hakuna watu wanao safiri kwa kutumia Meli.
Tuzidi kumwomba Mungu atuepushe na hili gonjwa linalosumbua dunia.
No comments:
Post a Comment