Wednesday, 29 July 2020
Monday, 27 July 2020
Saturday, 25 July 2020
TAARIFA YA POLISI LEO-POLISI LEO -OLE WAO WATAKAOFANYA MKUSANYIKO WOWOTE WA KUMPOKEA KIONGOZI WA CHADEMA TAREHE 27/07/2020
Polisi nchi nzima haina taarifa ya mkusanyiko wa kumpokea kiongozi wa chadema july 27/7/20 kama wanavyoelezana mitandaoni,Polisi tunatoa wito kwa wale wanaoitisha mikusanyiko bila ya kufuata sheria kwa makusudi watambue watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
POLISI
Rungu la sheria litawafuata wale wote watakaokusanyika
STEVE NYERERE KAULI MBIU YAKE BAADA YA KUSHINDWA KURA ZA KUTEULIWA UBUNGE NI WAJUMBE SIO WATU HAYA MANENO YANAZIDI KUMWEKA SEHEMU ITAKAYOLETA VISA KATI YAKE NA WAJUMBE.STEVE NAYE ALITOA RUSHWA INABIDI AHOJIWE NA TAKUKURU
Kama Steve Nyerere sasa hivi anahitaji wataalamu wa Saikolojia ili waweze kumsaidia kutokana na mazungumzo yake na Pierre ukiangalia Body Language hayupo sawa.
Tatizo limeanzia Iringa akisema Wajumbe sio watu wanasema hawajala chakula unawanunulia yaani hiyo ni Rushwa Takukuru inabidi kumuoji hawape ushahidi kwa nini alitoa rushwa
Friday, 24 July 2020
KAMPENI ZA RUSHWA TANZANIA KWA AJILI YA UCHAGUZI WA KUTEUA WABUNGE KATIKA KURA ZA MAONI NI SAWA NA KUMPIGIA MBUZI GITAA
Suala lingine ni Mameneja au watu wanaomwakilisha mtia nia kwa kuweza kuwashika wajumbe na huyo anayemwakilisha mgombea fulani yeye ndiye mshika pesa za huyo mtia nia na wajumbe kumfuata na kupata kitu kidogo hiyo ni kazi kuwakamata hawa watoa Rushwa.Nilikuwa na jamaa wakati wa uchaguzi wa kura za kumteua mgombea ubunge watu walikuwa wakitoka Dar es salaam kwenda mikoani kumfanyia kampeni mgombea aliyejipanga kupata Ubunge kupitia CCM sasa tujiulize kwa nini iwe hivyo?je huyo aliyechaguliwa kwa rushwa atakuwa kiongozi anayejali maslahi yako au maslahi yake?Kwa hali hiyo tunaomba Mwenyekiti wa taifa CCM na wajumbe wake wapitie hii hali na kuibadilisha CCM kuanzia mashinani ili kuboresha maendeleo ya chama.Kuna habari Mwenyekiti fulani anasaidia mjumbe fulani ili awe mbunge na wananchi wamekuja juu na kulalamika hiyo ndio hali tulionayo ya Rushwa kwa nini awe anasaidia mtu fulani?kazi ipo kwa kuweza kubadilisha CCM ambayo ina wajumbe Wapiga deal na kwa sababu uchaguzi kila baada ya miaka mitano basi tunasahau.Muhimu ni kwa chama kurekebisha haya matatizo yasije kutokea tena.
Tosamawe
HISTORIA YA MZEE MKAPA AMBAYE AMEFARIKI LEO KATIKA HOSPITAL MOJA JIJINI DAR ES SALAAM LEO 24-07-2020
Historia fupi ya Mzee Mkapa tuanz e na Urais.Alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania kuanzia Mwaka 1995 mpaka mwaka 2005.
Kuzaliwa 1938 Ndanda Masasi kusini mwa Tanzania.Alisoma shule ya msingi Masasi na kwenda Elimu ya sekondari katika shule ya Pugu alipokuwa akifundisha Mwalimu Julius K Nyerere ambaye alikujja kuwa rais wa kwanza wa Tanzania.
alienda Makerere na kumaliza degree ya kiingereza,pia alienda kwa masomo zaidi katika chuo cha Columbia na kupata Masters katika mambo ya diplomasia ya kimataifa.
Nyazifa alizowahi kufanya ni nyingi kama kuwa Waziri wa Sayansi na teknolojia na elimu ya juu.
Ameshika kazi katika balozi nje ya nchi Canada 1982 na Marekani mwaka 1983 mpaka 1984.
Alikuwa Waziri wa mambo ya nje kutoka 1977 mpaka mwaka 1980 na alirudishwa tena waizara ya mambo ya nje tena mwaka 1984 mpaka 1990.
Mungu aiweke roho ya marehemu Mzee Mkapa peponi Ameni.
TAARIFA YA MSIBA WA RAIS MSTAAFU MH BENJAMINI WILLIAM MKAPA AMBAYE AMEFARIKI LEO KATIKA HOSPITAL JIJINI DAR ES SALAAM
Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamini William Mkapa amefariki,Rais John Pombe Magufuliametangaza usiku huu kupitia Luninga ya taifa taarifa ya kufariki dunia kwa kiongozi huyo wa awamu ya tatu katika hospital moja jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwakwa matibabu
Mzee Benjamini Mkapa akiwa na Mama Mkapa
Mzee Benjamin akiwa na Mkewe Mama Mkapa katika sherehe yao ya Jubilee
Sunday, 19 July 2020
TOSAMAWE MATUKIO YA WIKI-CORONA VIRUS INAVYOSUMBUA DUNIA UCHUMI KUSHUKA NA NJAA KUWEPO MAELEZO YA WATAALAMU
Kutokana na janga kubwa lililozikumba nchi nyingi duniani ni kwamba sasa Uchumi unazidi kudidimia asa kwa zile nchi zinazotegemea misaada kutoka nje yaani nchi za dunia ya tatu.
Tukija kwenye uchumi wa nchi zilizoendelea wao wana mbinu nyingi za kuwasaidia watu wao kwa kuwapa msaada wa mikopo na pesa za kujikimu sasa kwa nchi za dunia ya tatu watu wanajiendesha wenyewe.
Utalii unazidi kudidimia kwa kasi kwa sababu Watalii wananogopa kusafiri na Oda zote zilizokwisha lipwa kwa ajili ya Utalii kwa mfano serikali ya \uingereza imewaambia Mawakala wa utalii kuwarudishia wateja wao pesa.Hii ni pigo kbwa kwa utalii kwa nchi nyingi zikiwemo za Afrika Asia na Amerika kusini.
Utalii wa kutumia Meli umeisha punguza wafanyakazi 200,000 ili kwendana na wakati kukiwa hakuna watu wanao safiri kwa kutumia Meli.
Tuzidi kumwomba Mungu atuepushe na hili gonjwa linalosumbua dunia.
Friday, 17 July 2020
Thursday, 16 July 2020
Wednesday, 15 July 2020
MHESHIWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ANAGOMBEA NAFASI YA KUTEULIWA ILI AWEZE KUWKILISHA WANANCHI WA WILAYA YA KIGAMBONI
Hatimaye mkuu wa mkoa wa dar es salaam awania jimbo la Kiganboni,hatua nzuri lakini anapingana na maagizo ya mkuu wake wa kazi aliyesema wakuu w mikoa wilaya bado wananhitajika kuwa kwenye nafasi zao.Hatakaye kihuka masharti atamtoa kwenye nafasi yake ya ukuu wa mkoa au wilaya.Sasa Makonda atenguliwa ukuu wa mkoa na kuwekwa mwingine.Hatuna wasiwasi Makonda atakuwa wa kwanza kupata hiyo nafasi na kuwakilisha wananchi wa Kigamboni.
Subscribe to:
Posts (Atom)