JAMBO LEO
Jeshi la Polisi Kanda Maalum DAR limesema wafuasi wa Askofu Gwajima
ni marufuku kutia mguu eneo atakalohojiwa Askofu huyo, ambapo kauli
hiyo imekuja siku chache baada ya Askofu huyo kuwataka wafuasi hao
kumsindikiza kuelekea kituoni hapo.
“Napenda
kutumia nafasi hii kumuomba GWAJIMA awaambie wafuasi wake hawahitajiki
kufika eneo hilo.. anayehitajika ni yeye na Mwanasheria wake”—Kamanda Suleiman Kova.
Kamanda Kova amesema iwapo kila mtu atafuata taratibu hakuna nguvu itakayotumika.
TANZANIA DAIMA
Vitendo vya wafanyabiashara kupigwa na
kunyang’anywa mali zao kwa kisingizio cha kusafisha Jiji vimezidi
kujitokeza ambapo ni kinyume na agizo la Waziri Mkuu Mizengo Pinda
ambaye aliwataka Wakuu wa Wilaya na Mikoa kukaa na wafanyabiashara hao
kuangalia namna watakavyofanya biashara zao ili kuondoa vurugu.
Waandishi wa Gazeti la TANZANIA DAIMA
walishuhudia Askari wa Jeshi la Polisi na Mgambo wakitembeza kipigo kwa
wamachinga kwa madai kuwa walikuwa wakifanya biashara maeneo ambayo
hayajaruhusiwa huku shuhuda mmoja akisema kwamba kashuhudia Askari hao
wakiwa na bunduki wakiwavamia na kuchukua bidhaa za wamachinga hao bila
kuziorodhesha kama inavyotakiwa.
“Tukio lile
lilikuwa halituhusu lakini kilichotukera ni kuona Askari ambaye
anategemewa kuwa mlinzi wa amani ndiye anakuwa wa kwanza kuvunja amani
kwa kuwapora wananchi mali zao tena kwa kutumia silaha”—alisema shuhuda huyo.
MWANANCHI
Askofu wa Kanisa Katoliki Mbeya amesema kama angekuwa na Mamlaka dhidi ya Waziri angemchapa makofi Waziri aliyeshindwa kutekeleza kauli ya kuzuia malori yanayoharibu barabara.
Askofu wa Kanisa Katoliki Mbeya amesema kama angekuwa na Mamlaka dhidi ya Waziri angemchapa makofi Waziri aliyeshindwa kutekeleza kauli ya kuzuia malori yanayoharibu barabara.
“Yupo
Waziri ambaye alisema malori makubwa yanaharibu barabara hivyo mizigo
yote inatakiwa kusafirishwa kwa Reli lakini mpaka sasa hajatekeleza..
kama ningekuwa na uwezo ningemchapa makofi” alisema Askofu Evarist Chengula.
Pamoja na kwamba Askofu huyo hakutaja jina la Waziri huyo lakini aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe
aliwahi kutamka kauli kama hiyo ambapo alipoulizwa kuhusu
kilichokwambisha kauli yake amesema kwamba ile haikuwa kauli yake ila ya
Serikali, hivyo wa kuulizwa kwa sasa ni Waziri husika Wizara hiyo
ambaye ni Samuel Sitta.
NIPASHE
Tukio la kujiua kwa askari Polisi wa kituo cha polisi Sikonge, Tabora, PC Charles Mkoyi limechukua
sura mpya baada ya ndugu kueleza utata wa majeraha aliyonayo ndugu yao
na malalamiko yaliyoelezwa na marehemu siku chache kabla ya kukutwa na
umauti.
Ndugu wa marehemu huyo wamedai kabla ya
kifo chake alilalamika kunyanyaswa na mmoja wa viongozi wa kituo hicho
tangu alipoingia kazini.
“Baadhi
ya malalamiko aliyotueleza ni kupangwa zamu zisizo na mpangilio, kwa
mfano, anakesha kazini badala ya kupumzika anatakiwa kurudi tena
kazini…muda mwingi alikuwa anachoka sana na hata alipolalamika hakuwahi
kusikilizwa na kiongozi huyo.”
Alisema utata unaanza Kituo cha Polisi
alichodaiwa alijipiga risasi kwa kuwa alitolewa haraka na kupelekwa
Hospitali ya Mkoa, huku picha zilizopigwa kwa ajili ya kuonyeshwa
familia na upelelezi, zikionyesha amekaa kwenye kiti akiwa amekumbatia
silaha.
“Tunavyofahamu
eneo lolote lenye tukio la mauaji kama hayo, mtu haruhusiwi kufika wala
kusafishwa hadi zipigwe picha na hata ndugu waone, lakini inaonekana
walimnyanyua na kumkalisha kwenye kiti na kumpiga picha, kwa muda mfupi
palisafishwa na mwili ukapelekwa Hospitali ya Mkoa. Tunajiuliza haraka
hiyo ya nini?” alihoji ndugu huyo.
Alisema kinachozua utata zaidi ni jinsi Charles
alivyojipiga risasi kwa kuwa inaonyesha risasi iliingilia nyuma na
kutokea mbele ambako kulikuwa na mfumuko mkubwa na nyuma tundu dogo,
jambo ambalo lina shaka kwa kuwa kwa uelewa wa kawaida anawezaje
kujipiga risasi kisogoni.
Ndugu hao walidai baada ya kufika kwenye
kituo hicho, walionyeshwa barua mbili zilizoandikwa na askari huyo,
moja ikiwa ya kikazi na nyingine ya familia na kwamba walisomewa kiasi
ya familia na ya kikazi haikusomwa na hawakupewa.
“Tunajua
mwili wa askari unaposafirishwa wanabeba na vitu vyake vyote, wanajua
alikuwa hajaoa, hana ndugu, wameacha vitu vyake vyote, kesho tunavunja
matanga ndiyo siku ya kugawana nguo za marehemu, kwa mazingira haya
tutagawana nini?” alihoji ndugu huyo.
Waliongeza kuwa hakukuwa na ukaribu wa polisi katika mazishi, alikuwa askari mwenzao lakini alizikwa kama raia wa kawaida.
Alisema walionana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Suzana Kaganda
na kumueleza malalamiko yote na kuahidi kuyafanyia kazi, huku akisema
ndani ya Jeshi la Polisi kuna utaratibu wa kufikisha malalamiko yoyote
yanayohusu askari wao.
“Waambie hao ndugu waje kuniona badala ya kulalamika kwenye vyombo vya habari,” alisema Kamanda Kaganda.
NIPASHE
Mkazi mmoja wa Kijiji cha Ulowa Kahama, Chausiku Hamis
ameuawa kwa kuchomwa moto na watu waliokusanyika katika msiba wa mtoto
wa jirani baada ya kutuhumiwa kuhusika na kifo cha mtoto huyo.
Mtoto huyo mwenye umri wa mwaka mmoja
alifariki usiku katika mazingira tata ambapo mwanamke huyo aliuawa baada
ya mmoja wa waombolezaji kupandisha mapepo na kumtuhumu Chausiku kuhusika na kifo cha mtoto huyo.
Diwani wa Kata hiyo amesema alipata
taarifa za mtoto huyo kuuawa na baadaye kuuawa mwanamke aliyetuhumiwa
kuhusika na tukio hilo ambapo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Mtendaji
wa Kitongoji hicho walikamatwa na Polisi baada ya nyumba za watu wote
kukimbiwa baada ya tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Shinyanga, Justus Kamugisha amethibitisha tukio hilo kutokea na kusema kuna watu wawili waliokamatwa kwa ajili ya upelelezi.
No comments:
Post a Comment