Waziri wa mambo ya nje wa Syria , Walid Maullem,
amesema anapinga vikali madai kuwa wanajeshi wa serikali ya Syria
walitumia silaha za kemikali.
Maullem, aliyasema hayo mjini Damascus, baada ya
Marekani kudai kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa silaha
za kemikali zilitumika nchini humo.Bwana Maullem, amesema wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, wameshindwa kufika katika eneo la pili linalodaiwa kushambuliwa kwa silaha hizo, baada ya kuzuiliwa na wapiganaji wa waasi.
Marekani na washirika wake wanajadili uwezekano wa kuanzisha mashambulio dhidi ya Syria kufuatia madai ya shambulio hilo la kemikali lililotokea wiki iliyopita.
Waziri huyo amewaambia waandishi wa habari, kuwa ikiwa nchi yake itashambuliwa kijeshi, kwa misingi ya kuwepo kwa silaha za kemikali, itakuwa kwa visingizio vya uongo na jambo ambalo halina msingo wowote.
Amekariri kuwa serikali ya Syria imetimiza ahadi zote ilizotoa kwa Umoja wa Mataifa kuhusiana na kuruhusu wachunguzi wake kufika nchini humo na pia kuwapa ulinzi
Awali serikali za Urussi na Uchina, kwa mara nyingine tena zimetoa onyo dhidi ya kutumia nguvu za kijeshi kutatua mzozo wa kisiasa unaokumba taifa la Syria.
Onyo hilo limetolewa huku Marekani na washirika wake wakijadili uwezekano wa kuanzisha mashambulio dhidi ya Syria, kujibu shambulio lililotokea wiki iliyopita
No comments:
Post a Comment