Saturday, 31 August 2013
Wednesday, 28 August 2013
TANZANIA INAHITAJI MAZOEZI MAKUBWA YA KIJESHI,KUNA SABABU YA UGANDA NA RWANDA KUJITOA KUTUMIA BANDARI YA DAR ES SALAAM.
Rais Museveni Uganda na Kagame Rwanda wanaSIRI yao.
Ninapenda kuzungumzia suala la usalama kwa upande wa nchi za maziwa makuu kama waswahili wanavyosema.Niliwahi kushiriki mkutano wa amani London katika jumba la bunge la Uingereza na kukutana na Profesa kutoka Kongo ambaye alizungumzia suala la Rwanda kushiriki katika mapigano ya Kongo.Suala lile lilileta hisia kali kiasi kwamba wenzetu weupe walimwita Profesa na kukaa naye kwa maelezo zaidi na kumtaja Kagame anavyotumia wakuu kuongoza waasi wa serikali ya Kongo.
MUHIMU KWA TANZANIA kuajiandaa kwa nguvu zote ili adui aone uwezo na sio kututania tania.Tujifunge mikanda tusione ni mchezo mchezo,hawa jamaa wawili ni marafiki au ndugu wa damu kwa hiyo tusifanye mchezo.
Tukumbuke pia ya IDD AMINI Nyoka ni kumkata kichwa tu kabla ajaruka na kukuuma
Katika mkutano huu ulitukutanisha watu kutoka mataifa mbalimbali na ulikuwa na maelezo ya watu wa Kongo wakiomba msaada kwa ajili ya kuwawekea vikwazo Museveni na Kagame.
Profesa katika picha hapo alikuwa akitafuta vielelezo na picha za viongozi wanaoendesha jeshi la waasi wa Kongo kutoka Rwanda.
SYRIA WAJIANDAA KWA KUJIBU MASHAMBULIZI KAMA WATASHAMBULIWA,WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA SYRIA WALID ASEMA KUNA NJIA MBILI ZA KUFANYA KAMA WATASHAMBULIWA 1-KUJIBU MASHAMBULIZI 2-KUJISALIMISHA.MAREKANI YAWEKA MAKAMBORA TAYARI KWA MIJI 50 KUSHAMBULIWA NA NDEGE KUANZA ALHAMISI MASHAMBULIZI.HATARI NYINGINE DUNIANI
Waziri wa mambo ya nje wa Syria , Walid Maullem,
amesema anapinga vikali madai kuwa wanajeshi wa serikali ya Syria
walitumia silaha za kemikali.
Maullem, aliyasema hayo mjini Damascus, baada ya
Marekani kudai kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa silaha
za kemikali zilitumika nchini humo.Bwana Maullem, amesema wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, wameshindwa kufika katika eneo la pili linalodaiwa kushambuliwa kwa silaha hizo, baada ya kuzuiliwa na wapiganaji wa waasi.
Marekani na washirika wake wanajadili uwezekano wa kuanzisha mashambulio dhidi ya Syria kufuatia madai ya shambulio hilo la kemikali lililotokea wiki iliyopita.
Waziri huyo amewaambia waandishi wa habari, kuwa ikiwa nchi yake itashambuliwa kijeshi, kwa misingi ya kuwepo kwa silaha za kemikali, itakuwa kwa visingizio vya uongo na jambo ambalo halina msingo wowote.
Amekariri kuwa serikali ya Syria imetimiza ahadi zote ilizotoa kwa Umoja wa Mataifa kuhusiana na kuruhusu wachunguzi wake kufika nchini humo na pia kuwapa ulinzi
Awali serikali za Urussi na Uchina, kwa mara nyingine tena zimetoa onyo dhidi ya kutumia nguvu za kijeshi kutatua mzozo wa kisiasa unaokumba taifa la Syria.
Onyo hilo limetolewa huku Marekani na washirika wake wakijadili uwezekano wa kuanzisha mashambulio dhidi ya Syria, kujibu shambulio lililotokea wiki iliyopita
MAGAZETI YETU LEO
- Wafanyakazi 1,076 watimuliwa Tazara
- CAG aisafisha wizara ya Magufuli
- Mnyika: Wananchi pazeni sauti tupate katiba nzuri
- `CCM ilichelewa kumchukulia hatua Mansour`
- Chadema kuweka hadharani maoni Rasimu Katiba keshokutwa
- Bomoabomoa yaacha kilio Mbezi Beach
- Waziri Kagasheki ambabua Meya
- Jeuri ya walimu:Huna Sh. 200 ya uji bakora
- Wabunge watuhumiwa kwa biashara dawa za kulevya
Monday, 26 August 2013
TANZANIA NCHI YETU INAPOCHEZEA BANDARI,SASA UGANDA NA RWANDA KUACHA KUTUMIA DAR PORT,WAZIRI WETU WA UCHUKUZI ANASEMA NI MWENDA WAZIMA ATAKAYEACHA KUTUMIA BANDARI YA DAR KWANI NI KARIBU UKITUMIA KENYA NI MBALI KWELI ATA KAMA KUNA MATATIZO WATUMIE TU KWELI TUPO PABAYA TUSUBIRI MADHARA YAKE YA AJIRA NA MAPATO,TUSUBIRI TENA CONGO,ZAMBIA NA MALAWI NAO WALIISHA SEMA WATATUMIA MSUMBIJI AU AFRIKA YA KUSINI
Dar es Salaam. Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania
(Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es
Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.
Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope
aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo
mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini
Serikali haikuchukua hatua.
MAGAZETI YETU LEO,WAUZA UNGA KUTAJWA BUNGENI HAAAAA KAZI HIPO POLISI,MAHAKAMA NIPO CHALINZE SIJUI NIENDE WAPI?
- Uda kuleta mabasi maalum kwa wanawake,
- Bomoabomoa yaacha watu 400 bila makazi,
- Uchimbaji holela wa mchanga watishia maendeleo ya wananchi,
- CCM yang`ang`ania serikali mbili,
- Utandazaji bomba la gesi Mtwara-Dar kuanza leo,
- Wauza `unga` kutajwa bungeni,
- Bomu lingine lakutwa kanisani D`Salaam,
- Mbowe, Lissu, Msigwa mbaroni,
- Wachimbaji wadogo waitaka TIB kuongeza kiwango cha mikopo,
Sunday, 25 August 2013
VITA,VITA NI BAADA YA MAJESHI YA SYRIA KUTUMIA SILAHA ZA SUMU,MAREKANI IMEISHA SOGEZA MELI ZAKE ZA KIVITA BAHARI NA KIONGOZI MMOJA WA JUU WA SERIKALI YA MAREKANI AMESEMA WATAANZA KUTUMIA MAKOMBORA YA MBALI KUHARIBU MIUNDO MBINU YA JESHI LA SYRIA.
Baraza la usalama la umoja wa
mataifa limefanya kikao cha dharura kujadili madai kwamba wanajeshi wa
serikali ya Syria wametumia silaha za kemikali pale walipofanya
shambulio dhidi ya eneo lililopo nje kidogo ya mji mkuu wa Damascus hapo
jana jumatano.
Wanaharakati wa upinzani wamesema kuwa mamia ya
watu wakiwemo watoto wameuwawa huku muungano wa upinzani ukiyataja
mauaji hayo ya halaiki. Serikali ya Syria imekanusha kwamba imetumia
silaha hizo.
Mwenyekiti
wa baraza la usalama, Maria Parceval, ambaye ni balozi wa Argentinean
katika umoja wa mataifa amesema kuwa wanachama wa baraza hilo wameelezea
wasiwasi wao kuhusiana na madai hayo.
"Naweza kusema kuwa kuna wasiwasi mkubwa
miongoni mwa wanachama wa baraza kuhusu madai hayo. Kuna hisia kwamba
kuna haja ya kuwa wazi kuhusu kilichotokea na hali kufuatiliwa kwa
makini,'' anasema Bi. Maria Parceval.
''Wanachama wote wanakubaliana kwamba matumizi
yoyote ya silaha za kemikali, kwa yeyote katika mzozo huu, na katika
mazingira yoyote ni ukiukaji wa sheria za kimataifa. Kulikuwa pia na
makubaliano ya kutoa wito wa kusitishwa uhasama na vita.''
Kadhalika Bi. Perceval amesema kuwa kulikuwa na makubaliano kuhusu haja ya kuanzisha uchunguzi wa kina kuhusiana na swala hilo.
''Wanachama wa baraza la usalama wametaka katibu
mkuu aingilie kati ili kuhakikisha kuwa uchunguzi wa haraka na wa kina
usioegemea upande wowote unafanywa. Wanachama wa baraza wameelezea haja
ya kutolewa mara moja msaada wa kibinadamu kwa waathiriwa. Hatimaye
baraza la usalama limetoa rambi rambi kwa waathiriwa pamoja na familia
zao,'' ameongeza kusema Bi. Maria Perceval, mwenyekiti wa baraza la
usalama la Umoja wa Mataifa.
Sunday, 18 August 2013
Saturday, 3 August 2013
Friday, 2 August 2013
MICHEZO BILA WATOTO AU VIJANA HATUNA TIMU HII NI BAKET BALL ENZI HIZO HII TIMU BAADAYE ILIWEZA KUCHUKUA KOMBE LA AFRIKA MASHARIKI NA KATI
Mpira au mchezo wowote unaanza kwa watoto aAmina Ahmed Hili
chama lilikua bonge la chama aisee...tulikua tunaingia uwanjani na
ngoma,wengine hadi tulikua tukirudi hme unakuta umesubiriwa mlangon
maana tulikua tukiomba ruhusa tukanyimwa bac tulikua tunatoroka,lolu vijana tunavyosema.Hii ilikuwa ni timu ya chini ya miaka 18 chini ya kocha Del ambaye baadaye ilikuja kuchukua komba la Afrika mashariki na kati basket ball.kuna mchezaji mmoja nimechukua Facebook
SIMBA NA YANGA WACHEZAJI WA AFRIKA MASHARIKI NDIO GUMZO LAKE,KWA NINI WASIWAANGALIE WA AFRIKA YA MAGHARIBI?
Afisa habari wa timu hiyo Ezekiel Kamwaga amesema kuwa beki wa kati Joseph Owino aliwasili nchini asubuhi ya leo na jioni hii amewasili beki Girbert Kazi kutoka burundi
kwa upande mwingine Kamwaga amesema kuwa taarifa za kusajiliwa na Yanga kwa kiungo mwenye kasi raia wa Uganda anayecheza soka nchini Vietnam Moses Oloya si za kweli kwani mchezaji mwenyewe amewahakikishia atatua katika timu hiyo
Subscribe to:
Posts (Atom)