KARIBU SANA TOSA MAWE BLOG KWA HABARI MBALIMBALI TOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA PIA TUTUMIE HABARI MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +447896103988 +447438590583 | E-mail: mwamfilingef@gmail.com NYOTE MNAKARIBISHWA SANA ASANTENI . | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US CLICK HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Saturday, 22 October 2011

KADAFFI ALIKUWA SHUJAA KAMA CHIFU WA WAHEHE MKWAWA

Kweli mtu aliyepitia JESHI ni lazima afe kishujaa maana Kadaffi amekufa kishujaa kwa sababu MJESHI
Binadamu yoyote duniani hapendi kuumbuliwa na ndio maana Chifu Mkwawa akupenda kukamatwa na wakoloni wa Kijerumani.
Kwa Kadaffi ili neno ninalolitumia nimelitoa kwa rafiki yangu kutoka visiwa vya Carribean aliniuliza umeona leo news mimi nilikuwa sijaona wala kusikia ndio akaniambia Kadaffi ameuwa leo ndio maana ninapenda kutumia neno hili Kadaffi ila ni Gadaffi.
Mfano mwingine ni Savimbi kutoka Angola yeye naye kwa sababu ni mjeshi naye alikimbia cheo cha umakamu wa Rais na kurudi msituni kupigana na alikuwa na pesa nyingi lakini kwa sababu ni Mjeshi basi naye aliuwawa kwa Risasi.
Tukirudi kwa rafiki yetu Gadafi naye alikuwa Rais lakini alipindua nchi kwa hiyo sifa ya mwanajeshi yoyote duniani kuuwa kwa mtutu wa bunduki ni USHUJAA kwa hiyo Gadaffi naye ni shujaa.
Tukiangalia nchi yetu nasi kila tarehe 1-9 kila mwaka tunakuwa na sikukuu ya mashujaa maana nao walifariki kishujaa.
Gadaffi wakati wa mapambano yake na waasi wake,aliambiwa na viongozi wa Afrika aende akaishi uhamishoni lakini yeye alikataa kwa kusema atapambana mpaka mwisho na sasa ni kweli mwisho wake umefika lakini amekufa kishujaa kwa bila kukamatwa na kupelekwa kwenye mahakama ya kimataifa ni kweli Gadaffi ni shujaa.Kiongozi mwingine wa Afrika yeye aliuwawa kwa mtutu wa bunduki ni Samuel Doe kweli ukiwa mwanajeshi ni lazima upambane hadi mwisho wake ndio utakuwa shujaa.
Nikiwa JKT afande wetu wakati wa mafunzo alituambia kwamba ukiwa vitani ni heri ufe kuliko kukamatwa mateka maana utateshwa kwa kukatwa vidole na adhabu nyingi kwa hiyo mwanajeshi kufa kkifo cha risasi ni ushujaa.
Gadaffi kweli nampongeza kwa kupigana mpaka mwisho wake maana ndo kazi ya MJESHI maana ya mjeshi ni mtu aliyepata mafunzo ya jeshi na kazi yake ni uanajeshi.
Mwisho nasema hapa duniani ni lazima kuelewa nguvu ya umma inaweza kukutoa madarakani hata kama una nguvu gani wewe kiongozi au wewe mtu unayeongoza watu hiwe ofisini au sehemu yeyote inayowakutaanisha watu wengi.
Asanteni.
The Quixotic Rise of Libya's Colonel Muammar Gaddafi
 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUPATA HABARI ZILIZOPITA BONYEZA OLDER POSTS