VITA KATI YA WAGANGA WA JADI WACHAWI NA SERIKALI NANI ATASHINDA?
KILA AKIPOTEA ALBINO WAGANGA NA WANAJIHUSISA NA BIASHARA YA VIUNGO HIVYO VYA ALBINO WAPELEKWE JERA.
POLISI mkoani Rukwa wanawashikilia watu
15, wakiwemo waganga wa kienyeji saba kwa tuhuma za kuhusika kwenye tukio la
kukatwa kiganja cha mtoto Baraka Cosmas.
Baraka (6), ambaye ni mlemavu wa ngozi,
alikatawa kiganja cha mkono mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akiwa amelala na
mama yake usiku.
Watuhumiwa hao walitiwa mbaroni kufuatia
msako mkali unaoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani hapa, ikiwa ni muda
mfupi baada ya tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob
Mwaruanda, alisema kikosi maalumu cha polisi kinaendelea na msako mkali
kuhakikisha mtandao wote wa utekaji na mauaji ya albino unatiwa mbaroni.
Alisema baada ya kutiwa mbaroni
watuhumiwa hao, walianza kutajana hadi kufikia 15, ambao wote kwa sasa
wanaendelea kuhojiwa kabla ya kupandishwa kizimbani kujibu mashitaka
yanayowakabili.
Kamanda Mwaruwanda aliwataja
wanaoshikiliwa kuwa ni Mwendesha William (30), Masunga Bakari (50), David
Kiyenze (45) na Ngolo Masinga (47), wote wakazi wa Kijiji cha Kaoze wilayani
Sumbawanga mkoani Rukwa.
Wengine ni Mageta Shimba (46), Pascal
Jason (40), Mnyika Managa pamoja na baba mzazi wa Baraka, Cosmas Yolam (32).
Waganga wanaoshikiliwa ni Eliza Malongo
(36), Sodeli Malimbo, maarufu kama Chuchi (66), Akobo Chinzwe (50), Leonard
Samson (59) na Inglibert Kasinde (45).
Wengine ni Boniphace Chalya (49), Charles
Misalaba (47) na Julius Simbamwene (40).
Alisema waganga wa jadi hao walikutwa na
vifaa vya kuagua na kupigia ramli pamoja na nyara za serikali kama vile mayai
ya mbuni, kucha za chui, ngozi ya pakapori, kobe aliyekaushwa, ngozi ya chui na
nywele zinazosadikiwa ni za binadamuMama wa mtoto aliyekatwa kiungo aliumizwa naye.
No comments:
Post a Comment