Aidha, Mheshimiwa waziri wangu Chana ambae ndiye Wizara yake inahusika na
watoto, kwa kuliona tatizo hilo la vyumba vya madarasa kuezuliwa alionyesha
kuguswa zaidi na hata kuwa kiongozi wa kwanza kuanza kuchangia mchango kwa ajili
ya harambee ya ujenzi wa vyumba hivyo kwa kuchangia kiasi cha Tsh 15,000/=
kupitia kwa mkuu wa shule hiyo Agnes Mageza ambaye pia kulingana na utaratibu wa
ukusanyaji wa fedha hizo na kuepuka matumizi yasiyotarajiwa na fedha za maafa,
alilazimika kuzipeleka fedha hizo kwa Afisa Mtendaji wa kijiji ili kuzihifadhi
kwa taratibu na kutoa stakabadhi kwa kila mchangiaji kama ilivyo taratibu za
upokeaji wa fedha za michago mbalimbali.
Pamoja na Waziri Pindi, Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe katika kuunga mkono jitihada za wapiga kura wake kwa wakati huo alipeleka saruji mifuko 50 ili kuanza kukarabati shule hiyo huku wananchi wakichangishana kiasi cha Tsh milioni 1.8 kati ya zaidi ya Tsh milioni 13 zilizokuwa zikihitajika ili kurejesha vyumba hivyo vya madarasa katika hali yake na watoto wapata kusoma.
Kasi ya michango kwa wananchi ilikuwa chini zaidi kwani hadi Desemba hii ni Tsh milioni 1.8 pekee na saruji mifuko 50 ndio iliyopatikana na kama kasi hiyo ingeendelea, hivyo hadi wananchi hao waweze kujenga vyumba hivyo kwa kupata Tsh milioni 13 basi ingekuwa ni mwakani mwezi Desemba.
Kwa kuliona hilo na uchungu wa maendeleo ya elimu kwa watoto hao mbunge Filikunjombe alilazimika kujitolea kujenga upya vyumba hivyo kwa zaidi ya Tsh milioni 13 ujenzi ulioanza Jumatatu wiki hii na wakati wa kujitolea kufanya hivyo Mkuu wa Shule hiyo, Bi Mageza na Katibu Tarafa ya Mawengi waliwashukuru wadau mbalimbali waliochangia akiwemo Waziri Chana aliyechagia Tsh 15,000.
Ajabu ni kwamba, baada ya vyombo vya habari kuripoti habari hiyo ya Waziri kupongezwa kwa kuchangia kiasi hicho cha fedha, Waziri Chana alinukuliwa akikana kuchangia maafa katika shule hiyo na hata kudai kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanamchafua
No comments:
Post a Comment