Damas Makangale, Mhariri MOblog
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa mara nyingine tena ameibuka na kauli ambao alishawahi kuitoa huko nyuma ya viongozi wa Serikali ya awamu ya nne kushidwa kuchukua uamuzi mgumu kwa maslahi mapana ya taifa.
Lowassa alitoa kauli hiyo mjini Dodoma katika kikao cha bunge kinachoendelea akisema nchi inakosa viongozi jasiri wenye kusimamia utekelezaji wa mambo waliyoamua katika Nyanja mbalimbali za maendeleo.
"wananchi, wanasiasa, wabunge, viongozi wanalalamika hatuwezi kuwa na jamii ya kulalamika lazima mtu mmoja ajitokeze na kufanya maamuzi magumu lazima ajivishe joho la ujasiri ili mambo yaende,' amesema Lowassa.
Amesema nchi ina tatizo kubwa la uswahili mwingi wa kukaa na kushidwa kutekeleza mambo yaliyoamualiwa kwenye vikao kiasi cha kufanya kila mtu kulalamika kwa wakati wake
Lowassa amesema kuwa hata matokeo makubwa sasa au "Big results Now" haiwezi kutekelezwa kwa sababu ya uswahili na mazingira ya hapa Tanzania na Malaysia ni tofauti hapa ni uswahili tu ndio unaosumbua taifa letu lishindwe kusonga mbele.
"Tukishakubaliana mambo ni lazima yafanyike. Ni lazima tuondokane kuwa nchi ya kulalamika kuanzia kiongozi wa juu mpaka mwananchi," alisisitiza
Sisi katika Moblog tunaungana na Lowassa katika kutekeleza mipango ya serikali kama ilivyopangwa bila woga wala kigugumuzi lazima viongozi wote waliopewa dhamana ya kuongoza waongoze kwa vitendo waache uswahili ili taifa liweze kusonga mbele.
Tunakubaliana naye kwa sababu, siku za hivi karibuni tumeona wamiliki malori wakikataa kulipa tozo ya asilimia tano kwenye mizani ya serikali wakati sheria ya ongezeko la asilimia hizo tano lilipitishwa na bunge na waziri mwenye dhamana John Pombe Magufuli alikuwa sahihi kwa kusimamia sheria lakini kawa kawaida Magufuli alipigwa stop na viongozi wake kwanini? Sheria za nchi hazifuatwi yale yale uswahili.
Lowasa ambaye ni mbunge wa Monduli (CCM) amesema kuwa ni vema serikali ingekuwa na mipango michache yenye kutekelezeka na tija kwa taifa.
Aliongeza kuwa kama angekuwa kiongozi wa serikali angejikita kwenye vipaumbele vitatu ambavyo ni ajira, Reli ya Kati na elimu kuliko kuwa na vipaumbele vingi visivyotekelezeka.
Alibainisha kuwa tatizo kubwa linaloifanya serikali ishindwe kufanya vizuri kwenye maeneo mbalimbali ni kujiwekea vipaumbele vingi huku rasilimali zake zikiwa chache na wakati mwingine zile zinazopatikana hazitumiwi vizuri.
No comments:
Post a Comment