KARIBU SANA TOSA MAWE BLOG KWA HABARI MBALIMBALI TOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA PIA TUTUMIE HABARI MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +447896103988 +447438590583 | E-mail: mwamfilingef@gmail.com NYOTE MNAKARIBISHWA SANA ASANTENI . | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US CLICK HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Friday, 18 January 2013

JAMII FORUM RAIS HASHINDWA KUELEZEA MAUAJI YA RAIA YANAYOFANYWA NA POLISI KWA WANADIPLOMASIA KATIKA TAFRIJA


Mauaji ya raia ambayo yanajirudia, katika tafrija kama hiyo ambayo ilifanyika mwaka 2011/12 Rais Kikwete alitamka na kuapa mbele ya Mabalozi kwenye tafrija iliyofanyika Ikulu kwamba mauaji kama hayo katu hayatatokea tena, serikali itafanya kila liwezekanalo hayo yasitokee tena. Nanukuru: "Nawahakikisheni waheshimiwa mabalozi, mauaji ya raia hayatatokea tena, serikali itafanya kila liwezekanalo kuzuia mauaji yasitokee." Leo duniani hadi mahakama ya kimataifa mafaili yaliyosheheni picha mbaya za mauaji ya raia yanayofanywa na polisi zilizoambatanishwa kama ushahidi wa mashtaka dhidi ya serikali ya Kikwete yanamtia kugugumizi kutamka tena mbele ya wanadiplomasia aliowaahidi.

Moja ya kauli ya Kikwete kwamba sakala la gasi Mtwara inatumiwa na wanasiasa kama hoja ya kujiimarisha imefunika mengi ambayo yametokea wiki moja kabla ya tafrija aliyowafanyia mabalozi Ikulu kuukaribisha mwaka mpya kama ilivyoada. Yapo mengi kichwani ambayo vigumu na pengine kupata kigugumizi kuyaongelea kama:
  • Ufisadi serikalini
  • kuficha pesa Uswis
  • Senator ya Marekani kumtuhumu kuvunja haki za binadamu katika utawala wake kwa polisi kuua raia bila kukemea
  • Kufikishwa mahakama ya haki za binadamu duniani suala la mauaji ya raia yanayofanya na chombo cha serikali ambacho ni polisi
  • Mtafaruku wa ardhi
  • Kutorosha wanyama
  • Mikataba feki nk
  • Utoroshwaji wa madini

  • Pengine ameona aibu kutamka kitu alichoahidi na leo mambo ni mabaya zaidi. Badala yake ametumia tukio la gas Mtwara kama kivuli na mahali pa kujenga hoja ya kuwasema vyama vya upinzania, ambapo katika kampeni za uchaguzi Mkuu uliopita alisema ni vyama vya msimu, leo vinamtesa anakosa usingizi hadi kuweka kando sera za CCM nyingi zisizotekelezeka na kuamua kutumiwa na vyama vya upinzania hasa Chadema kutekeleza sera zake kama suala la katiba mpya.

      No comments:

      Post a Comment

      Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
      KUPATA HABARI ZILIZOPITA BONYEZA OLDER POSTS