Rais wa Marekani Barrack Obama, amewataka wabunge wa bunge la
wawakilishi kupitisha maazimio yaliopitishwa na bunge la Senate kuhusu sera mpya
ya uchumi bila kusita.
Bwana Obama, amesema kuwa makubaliano hayo yanawaokoa asili mia sabini ya
Wamarekani dhidi kupandishiwa ushuru na pia yataimarisha uchumi uchumi waa taifa
hilo.
Rais Obama, amesema kuwa kwa mara ya kwanza wanaomiliki mabilioni na
mamilioni ya fedha watalazimika kulipa ushuru unaohitajika kwa mara ya kwanza
kwa zaidi ya miaka ishirini iliyopita.
Wabunge wa chama cha Republican, wamesema kuwa watahitaji muda zaidi kusoma
mapendekezo hayo.
Hata hivyo wantarajiwa kupiga kura baadaye hivi leo.