Alhaj Ismail Aden Rage ambae ni mbunge wa Tabora mjini amesema anatambua kila kinachoendelea ndani ya klabu kwa kusema kuwa wapo wanaosababisha hali hii itokee lakini yapo mengi ambayo yamebadilika katika utawala wake.
Kwenye sentensi ya pili amesema kwa niaba ya uongozi wa klabu ya Simba anapenda kuchukua fursa hiyo kumuomba radhi nahodha na mlinda mlango wa klabu ya Simba Juma Kaseja kwa yote yaliyomsibu baada ya mechi dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo kwa sasa moja kati ya mambo ambayo uongozi wake umepania kuyafanya ni kuitoa timu nje ya nchi kwa matayarisho ya duru ya pili ya ligi kuu na mashindano ya kimataifa.
Rage pia alizungumzia ishu ya kusimamishwa uanachama wanachama Ally Bane na Ustadh Masoud kwa kile alichokiita kukiuka katiba ya klabu ya Simba kutokana na walichofanya ikiwemo kuhamasisha wanachama wa Simba kutia saini ili kikao cha dharura kifanyike kuokoa migogoro iliyopo kwenye klabu wakati huu.
Pia mwenyekiti huyo amevunja kamati ndogo zote alizoziteua kipindi kilichopita ambazo ni kamati ya mashindano inayoongozwa na Joseph Itang’are Kinesi, ya Ufundi iliyokuwa ikiongozwa na Ibrahim Masoud, kamati ya fedha iliyokuwa chini ya Geofrey Nyange Kaburu, kamati ya usajili iliyokuwa chini ya Zakaria Hanspope na kamati ya nidhamu.
No comments:
Post a Comment