KARIBU SANA TOSA MAWE BLOG KWA HABARI MBALIMBALI TOKA PANDE ZOTE ZA DUNIA | TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA PIA TUTUMIE HABARI MATUKIO KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NASI KWA SIMU: +447896103988 +447438590583 | E-mail: mwamfilingef@gmail.com NYOTE MNAKARIBISHWA SANA ASANTENI . | DO YOU NEED TO CREATE BLOG CONTACT US CLICK HERE | UNAHITAJI KUFUNGUA BLOG WASILIANA NASI BOFYA HAPA

Friday, 30 November 2012

PALESTINA NJIA NZURI YA KUTAMBULIKA DUNIANI LAKINI MMMM

Palestina na madai yao sasa wapewa nafasi ya kuwa nchi mwangalizi wa Umoja wa mataifa lakini kupewa huko nafasi bado kuna vitendawili vingi ninavyojiuliza na wataalamu wengi duniani wanalizungumzia kwa undani,nimesikiliza Aljazeera tv na Magazeti mbalimbali kwangu ninaona kama CHANGA LA MACHO.
-Marekani wanalipinga na baadhi ya nchi za magharibi wakiwaambia Wapalestina wazungumzie      Amani na Israel.Kutokana na Palestina kutoitambua Israel ni tatizo litakalo dumu kwa muda na mwisho wake ni Vita.
-MUHIMU ni Nini kitafuata baada ya Palestina kuwekwa kwenye Umoja wa Mataifa maana hawawezi kuwepo kwenye Mahakama ya Kimataifa.
KWA UFUPI BADO NI SAFARI NDEFU TUOMBE MUNGU ILI AMANI IPATIKANE KWANZA. 

HALI YA HEWA KWA ULAYA BARIDI IMEANZA LEO ASUBUHI -2C NA JUMAPILI NDIO ITAKUWA BARIDI KALI ZAIDI


Usiku na Asubuhi hali ilikuwa hivi,watu na ususani watoto wanangojea kwa furaha barafu ishuke na waanze kutengeneza Snow Man wengine wanasikitika bili za Gesi na Umeme kuongezeka.





MAGAZETI YETU LEO





 

PENDA SEHEMU YAKO ULIYOZALIWA HATA KAMA KUNA NYUMBA ZA NYASI,MCHEZAJI WA BASKETBALL KUTOKA DODOMA ALINITUMIA HII PICHA


Thursday, 29 November 2012

TWANGA PEPETA NINAVYOIPENDA NITAKUNYWA SUMU JUU YAKE.INANIKUMBUSHA MBALI


SHULE SHULE SHULE HEEE


MAGAZETI YETU YA LEO



WAAFRIKA NA MAWAZO MGANDO,KWANI OBAMA NI RAIS WA AFRIKA AU MAREKANI,NIMEONA KWENYE FACEBOOK NA MAGAZETI MBALIMBALI YAKIMWELEZEA OBAMA KAITUPA AFRIKA! KUNA SERA ZA KUSAIDIA NCHI SIO OBAMA ATATOA MSAADA KWA AFRIKA KWA SABABU NI MWAFRIKA.

Je Obama atapuuza Afrika tena?


 

Obama na mkewe Michelle

Kuna baadhi ya wenyeji wa bara hili waliotegemea mengi zaidi kutoka kwa mwanawe mtu aliyekuwa akichunga mbuzi huko Magharibi mwa Kenya
Lakini Rais Barack Obama, katika muhula wake wa kwanza, alizuru Afrika mara moja tu, tena kama mpita njia, na kusema wazi kwamba hangekuwa anajihusisha kupita kiasi na maswala ya Afrika.
“Hatima ya Afrika iko mikononi mwa Waafrika wenyewe,” alisema huko Ghana, katika hotuba iliyodhihirisha wazi kwamba ushawishi wa Marekani unapungua katika bara ambalo sasa linafanya biashara zaidi na Uchina kuliko Marekani.
Kwa hivyo, ni mabadiliko yapi yatakayokuwepo katika muhula wa pili?
“Kama Kenya itafanya uchaguzi huru, basi Obama ataitembelea nchi hiyo.''
Swala hili la yeye kutokuwa na muda na Afrika, kwa sababu ya matukio mengine, halikutiwa mkazo katika uchaguzi ulioangazia maswala nyeti nchini Marekani na harakati za mapinduzi katika nchi za Kiarabu.
Akitoa hotuba yake baada ya kushinda, Bwana Obama aligusia tu “,muongo wa vita” na “watu walioko katika nchi za mbali… wanaoweka maisha yao hatarini ili tu kujadili masuala muhimu, na kupata nafasi, kama sisi, kupiga kura kama sisi tulivyopiga leo”
Hakuna “Kanuni za Obama”
Katika muhula wa kwanza, maswala yalilenga mizozo mikubwa iliyokuwa Ivory Coast, Somalia, Sudan and Sudan Kusini, na hata uchaguzi uliofanywa Zambia.
Kuna uwezekano kwamba mwanzo wa muhula wa pili atajishughulisha na masuala kama hayo: mikakati ya kimataifa kuwaondoa waasi wenye uhusiano na Al-Qaeda kutoka Mali kaskazini – kwa kutumia nguvu au mazungumzo, au yote mawili – na juhudi kuhakikisha kuwa Zimbabwe na Kenya hawatakuwa tena na michafuko baada ya uchaguzi, iliyoharibu chaguzi zao zilizopita.
Hadi sasa, hakujawa na ishara yoyote ya kuwepo kwa “Sera Kabambe ya Obama” kwa ajili ya Afrika. Labda hilo siyo jambo baya ukitilia maanani tofauti na masuala mengine kuhusu Afrika.
Rais Barack Obama mjini Washington

Bwana Obama kawaachia wengine watoe tahadhari kuhusu Uchina, nchi ambayo haijitoshelezi kirasilimali.
Lakini kuna uwezekano kwamba muhula wake wa pili utampa nafasi ya kujiondoa kutoka kwa mkakati wake wa “vita dhidi ya ugaidi” huko Mali na Somalia, na kuangazia maswala mapana zaidi – hususan biashara – jambo aliloligusia miaka mitatu iliyopita nchini Ghana.
Chanzo BBC swahili news.

Thursday, 22 November 2012

KLABU BINGWA YA MPIRA ULAYA NI FUJO FUJO BAADA YA WAPENZI WA MPIRA WA TIMU YA TOTTEHAM KUTOKA LONDON UINGEREZA KUPIGWA KWENYE BAR NA WAHUNI WA TIMU YA LAZIO YA ITALIA




MBUNGE WA CONCERVATIVE ALIYEFUNGIWA NA CHAMA CHAKE BAADA YA KWENDA KUSHIRIKI KAMBI YA I,AM CELEBRITY AUSTRALIA HATOLEWA KWA KURA ZA WANANCHI

Mbunge Nadime wa Tory waziri wake mkuu David Cameron ametolewa kwenye kinyang'anyiro cha I am celebrity.Amesikitika lakini hajutii kufungiwa na chama chake kwa muda.

TAJIRI WA CHELSEA ANAVYOBADILISHA MAMENEJA WA TIMU YAKE YA CHELSEA BILA KUWASIKILIZA WAPENZI WA CHELSEA.

Abromovich pichani ameisha wafukuza makocha wake kumi 10 tangu anunue timu ya Chelsea.Di mateo alikuwa sio chaguo lake ila wapenzi walimlazimisha kumchukua baada ya kutwaa ubingwa wa Ulaya.Nafikili Abrmovich yeye anataka Chelsea icheze kama Barcelona au Real Madrid mpira safi kabisa,sio mpira wa kubutua butua.Yetu Macho.

SHAMBULIZI LA ISRAELI KWA WAPALESTINA LINATISHA.NINA KITABU CHA MAMBO YA VITA NA ULINZI KITABU KINAITWA SPACEWARFARE AND STRATEGIC DEFENCE.WAISRAELI WANAZANA ZA KUJILINDA NA MAKOMBORA KAMA HAYO YALIYOPO KWENYE KITABU.

Shambulizi hili  limenisikitisha baada ya kuliona kwenye Tv jinsi kombora lilivyopiga likalipuka mara Tatu na kubakiza shimo hilo limeua watu 9 wa familia moja watu  wawili majirani na mtu mmoja amepona katika shambulio hilo.

CHADEMA NA FUKUZAFUKUZA YA MADIWANI,IFIKE WAKATI WA KUWAFUNZA WANACHAMA WAO MAADILI YA UONGOZI.NI VYEMA KUWAFUKUZA WATU WASIO WATII WA MAAMUZI LAKINI CHADEMA WAELEWE WATANZANIA BADO HAWANA UWEZO WA KUTAMBUA UOVU WAO WANASHABIKIA ZAIDI UPEPO UNAPOKWENDA.


Sunday, 18 November 2012

ISRAEL NA PALESTINA HAMAS MAKOMBORA,MABOMU NA BUNDUKI SIO NJIA YA KUMALIZA VITA.MWENDENI KWENYE MAZUNGUMZO.

Kombora kama hili linawaumiza watoto na mama wajawazito. 

Makombora sio njia ya kumaliza vita ni mazungumzo tu.

Bunduki hazitasaidia utulivu ni mazungumzo ya amani tu ndio jibu.

WAPENZI WA SIMBA WANAVYOTUMIA NGUVU YA UANACHAMA KUWAPINGA VIONGOZI AU WACHEZAJI.ADEN RAGE ALONGA KINACHOENDELEA SIMBA

 



 
ADEN RAGE
Wakati kukiripotiwa kuwa na hali isiyo nzuri ndani ya makao makuu ya klabu ya Simba kutokana na matokeo ya hivi karibuni kwenye ligi kuu Tanzania, mwenyekiti wa klabu hiyo Aden Rage amekaa na kuzungumza na waandishi wa habari.
Alhaj Ismail Aden Rage ambae ni mbunge wa Tabora mjini amesema anatambua kila kinachoendelea ndani ya klabu kwa kusema kuwa wapo wanaosababisha hali hii itokee lakini yapo mengi ambayo yamebadilika katika utawala wake.
Kwenye sentensi ya pili amesema kwa niaba ya uongozi wa klabu ya Simba anapenda kuchukua fursa hiyo kumuomba radhi nahodha na mlinda mlango wa klabu ya Simba Juma Kaseja kwa yote yaliyomsibu baada ya mechi dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo kwa sasa moja kati ya mambo ambayo uongozi wake umepania kuyafanya ni kuitoa timu nje ya nchi kwa matayarisho ya duru ya pili ya ligi kuu na mashindano ya kimataifa.
Rage pia alizungumzia ishu ya kusimamishwa uanachama wanachama Ally Bane na Ustadh Masoud kwa kile alichokiita kukiuka katiba ya klabu ya Simba kutokana na walichofanya ikiwemo kuhamasisha wanachama wa Simba kutia saini ili kikao cha dharura kifanyike kuokoa migogoro iliyopo kwenye klabu wakati huu.

Pia mwenyekiti huyo amevunja kamati ndogo zote alizoziteua kipindi kilichopita ambazo ni kamati ya mashindano inayoongozwa na Joseph Itang’are Kinesi, ya Ufundi iliyokuwa ikiongozwa na Ibrahim Masoud, kamati ya fedha iliyokuwa chini ya Geofrey Nyange Kaburu, kamati ya usajili iliyokuwa chini ya Zakaria Hanspope na kamati ya nidhamu.

MAGAZETI YETU LEO JUMAPILI






DK SLAA AICHAMBUA CCM

 

ADAI WATEULE WAPYA WANA TASWIRA YA UFISADI
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ameichambua safu mpya ya uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyoundwa hivi karibuni mjini Dodoma, akisema wana taswira ya ufisadi.
Amesema kuwa hali hiyo inatokana na baadhi yao kuhusika kwenye matukio kadhaa ya kifisadi moja kwa moja.
Akizungumza na Tanzania Daima jana kuhusu mtazamo wake kwa safu hiyo mpya ya uongozi wa CCM iliyoundwa na Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, katika mkutano mkuu uliomalizika juzi, Dk. Slaa alisema haoni jambo jipya.
“Nadhani hakuna jambo jipya, kipya ni kwamba wameteuliwa jana, lakini wote ni wazoefu wachafu,” alisema.

ISRAEL WASHAMBULIA OFISI ZA WAZIRI MKUU WA HAMAS, JENGO LILILOSHAMBULIWA LIKIONEKANA KAMA SHIMO


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
KUPATA HABARI ZILIZOPITA BONYEZA OLDER POSTS